Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAHARUSI WAZUA GUMZO KUPANDA NDANI YA KEKI KUBWA YENYE MUUNDO WA GARI..Tazama Video Hapa


Wanandoa wamewasha moto mtandao na video za keki waliyotumia katika hafla yao ya harusi ikisambaa mitandaoni.

Wanandoa waliamua kuipa hafla yao ya harusi ladha ya kipekee na yenye kumbukumbu kutokana na aina ya keki waliotumia

Wanandoa hao ambao wanasemekana kuwa raia wa Ghana, walinaswa kwenye video iliyopakiwa na Live Weddings kwenye Instagram wakiwa wameketi ndani ya keki hiyo yenye muundo wa gari.

 Wanandoa hao wanaonyeshwa kwenye video wakiwa wameketi ndani ya keki hiyo yenye rangi nyeupe pepepe, na kisha walipeana busu tamu

 Keki hiyo iliyokuwa imepambwa na kupambika ingeweza kufafanishwa na gari la kawaida kama ingelikuwa na mataa.

Wakiwa humo ndani, bwana harusi alishikilia keki hiyo na nguvu huku akibusiana na bibi harusi wageni wakishangilia na furaha. 

Keki hiyo inadaiwa kugharimu mamilioni ya pesa. Sawia na wageni katika harusi hiyo, wanamtandao hao walionekana kuduwazwa na keki hiyo huku wakiwasherehekea maharusi hao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com