RC MJEMA AFUNGA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA..ATAKA UKAGUZI MAKAMPUNI YA ULINZI


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akizungumza kwenye ufungaji wa mafunzo ya Jeshi la Akiba mkoani humo.


Na Marco Maduhu, Shinyanga

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, ameagiza ufanyike ukaguzi kwenye Makampuni ya ulinzi mkoani humo, na kuwaondoa walinzi ambao hawajapitia mafunzo ya kijeshi, hawajui kutumia silaha huku wengine wakilala lindoni.

Mjema amebainisha hayo leo Ijumaa Oktoba 29,2021 wakati akifunga mafunzo ya wahitimu wa Jeshi la Akiba mkoani humo wapatao 186, zoezi ambalo limefanyika kwenye viwanja vya Ndembezi jirani na Ofisi ya Kata, na kuhudhuriwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, Maofisa wa Jeshi, viongozi wa Serikali , Chama cha Mapinduzi na wananchi.

Amesema Makampuni mengi ya ulinzi mkoani humo yameajiri walinzi wasikokuwa na sifa, ambao hawajui kutumia silaha huku wengine wakisinzia lindoni, jambo ambalo ni hatari kwenye masuala ya kiusalama, ikiwamo ulinzi wa Raia na mali zake.

“Vijana wetu hapa wamehitimu mafunzo ya Jeshi la Akiba na wanajua vizuri kabisa kutumia Silaha, lakini ukienda kwenye makampuni ya ulinzi, unakuta mlinzi ana Silaha lakini hajui hata kuitumia “siku moja nilimkuta mlizi ana linda nikamuuliza una jua kuitumia silaha, akasema hajui, nikaamuuliza sasa akija mharifu unaitumiaje akasema hivyo hivyo tu itapigwa,”alisema Mjema.

Aliongeza kuwa mlinzi ambaye hajapewa mafunzo ya kijeshi hapaswi kupewa kumiliki Silaha, sababu ataweza kuuwa watu wengine ambao hawatakiwi kuuawa, ikiwa mambo mengi ya kijeshi hayajui wala nidhamu ya kuwa na Silaha, na wengine ukiwakuta kwenye lindo wameweka miguu juu, na wengine wamelala kwenye vibanda.

“Naagiza Wakuu wa wilaya na Jeshi la Polisi myachunguze Makampuni haya ya ulinzi, na kuondoa walinzi ambao hawajapitia mafunzo ya kijeshi, na Kampuni ambazo zitakataa kutii magizo ya Serikali zifungeni,”aliongeza Mjema.

Katika hatua nyingine amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashuri mkoani Shinyanga, kuwatumia vijana wa Jeshi la Akiba kwa kuwapatia vibarua kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ukiwamo ujenzi wa vyumba vya madarasa, sababu vijana hao ni Wazalendo, Watiifu, na Waaminifu, na hawataweza kufanya wizi wowote ule, ambapo Mchanga,Saruji,kokoto vyote vitatumia vizuri.

Pia amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, kwa kuajiri vijana 33 ambao wamehitimu mafunzo hayo ya Jeshi la Akiba, kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali za Serikali, na kuomba Wakurugenzi wote mkoani humo wawapatie nafasi vijana hao.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amewataka wahitimu hao, mafunzo ambayo wameyapata wakayatumie vizuri kwa ujenzi wa Taifa, ikiwamo kulinda usalama wa Raia na Mali zao, pamoja na kushiriki kikamilifu kwenye shughuli mbalimbali za kiserikali.

Kaimu Mshauri wa Jeshi la Akiba mkoani Shinyanga Meja Ford Mwakasege, akisoma Taarifa ya Mafunzo hayo, alisema yalianza June Mwaka huu na kuhitimishwa leo, ambapo jumla ya wahitimu 186 wamemaliza mafunzo yao wanawake 35 na wanaume 151.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza wakati wa ufungaji mafunzo ya Jeshi la Akiba mkoani ni humo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye ufungaji wa mafunzo ya Jeshi la Akiba.
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Ester Makune, akizungumza kwenye ufungaji wa mafunzo ya Jeshi la Akiba.

Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Agnes Bashemu akizungumza kwenye ufungaji wa mafunzo ya Jeshi la Akiba.

Diwani wa Vitimaalum Manispaa ya Shinyanga Zuhura Waziri akizungumza kwenye ufungaji wa mafunzo ya Jeshi la Akiba.

Kaimu Mshauri wa Jeshi la Akiba mkoani Shinyanga Meja Ford Mwakasege, akisoma Taarifa ya Mafunzo hayo.

Wahitimu wa Jeshi la Akiba.

Wahitimu wa Jeshi la Akiba.

Wahitimu wa Jeshi la Akiba.

Wahitimu wa Jeshi la Akiba.

Wahitimu wa Jeshi la Akiba, wakitoa burudani.

Viongozi wakiwa meza kuu wakiangalia burudani kutoka kwa wahitimu wa Jeshi la Akiba.

Wananchi na wazazi wakiangalia vijana wao wakihitimu mafunzo ya Jeshi la Akiba.

Wananchi na wazazi wakiangalia vijana wao wakihitimu mafunzo ya Jeshi la Akiba.

Viongozi wakipiga picha ya pamoja na wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Akiba.

Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.

Picha za pamoja zikipigwa viongozi na wahitimu wa Jeshi la Akiba.

Na Marco Maduhu- SHINYANGA.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post