Dkt. Sawanda Soko
Na Frankius Cleophace Tarime.
Wazazi wameaswa kunyonyesha maziwa watoto wao angalau mara kumi au zaidi kwa siku ili kuimarisha suala la Lishe kwa watoto ili kuepuka udumavu.
Hayo yamebainishwa na Dkt. Sawanda Soko kutoka Kituo cha Tiba asilia kwa njia ya mimea, matunda,mbogamboga na maua wilayani Tarime Mkoani Mara wakati akizungumzia siku ya Lishe kitaifa ambayo hufanyika kila ifikapo Oktoba 23 kila mwaka.
Sawanda alisema kuwa mtoto kuanzia miaka sifuri nakuendelea katika makuzi yake lazima mama amnyonyeshe maziwa pekee kwa kipindi cha miezi sita bila kupewa kitu chochote ili kumjenga kiafya.
“Kitalaamu mama anapaswa kunyonyesha mtoto kwa siku zaidi ya mara kumi au mara kumi na mbili kwa sababu maziwa ya mama yamebeba virutubisho vyote ili mtoto hasiweze kupata udumavu”, alisema Sawanda.
Vile vile Sawanda aliongeza kuwa baada ya kunyonyesha pale mtoto anapoanza kula chakula anapaswa kupewa uji kwa kipindi cha miezi mitatu na badaae ndipo apewe chakula mfano ndizi zikiwa zimepondwa au kusagwa kwa kuchanganya na samaki ili kuboresha lishe kwa mtoto.
Kwa upande wake Mratibu wa Masuala la Lishe katika Halmashauri ya Mji wa Tarime Mkoani Mara Monica Ouk alisema kuwa suala la elimu juu ya matumizi ya chakula sahihi kwenye jamii inaendelea kutolewa ili kupunguza udumavu wa watoto.
Katika hatua Nyingine akitoa maoni juu ya umhimu wa lishe suala la chakula shuleni hususani wanafunzi wa awali linatajwa ambapo Peter Mwita kutoka kituo cha kutoka kituo cha Maendeleo ya kilimo na ushari Mogabiri kupitia kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tarime alisema kuwa kama kituo wameanzisha sualala uji shuleni kwa baadhi ya shule jambo ambalo limechochea ufaulu kwa wanafunzi nakuomba wazazi na walezi kuchangia chakula shuleni.
Kauli Mbiu ya Mwaka huu katika kilelele cha siku ya Lishe kitaifa inasema kuwa “Lishe Bora ni Kinga Thabiti dhidi ya Magonjwa, Kula Mlo Kamili , Fanya Mazoezi, Kazi Iendelee na maadhimisho hayo kitafifa yamefanyika hii leo Oktoba 23 Mkoani Tabora