BINTI mwenye umri wa miaka 21, ambaye ni mama wa watoto 2, amejiua kutokana na msongo wa mawazo uliosababishwa na kutelekezewa watoto wawili bila ya msaada wa malezi kutoka kwa mzazi mwenzake.
Kabla ya kifo chake mwanamke huyo aliweka post kadhaa kuelezea hali aliyokuwa anapitia kichwani mwake. Olivia Popham raia wa Marekani alijizolea umaarufu mkubwa kupitia mtandao wa Tik Tok na instagram kutokana na uzuri wake, alifahamika kwa jina la Livi Jaay.
Binti huyo aliamua kuliingiza gari lake kwa makusudi mbele ya roli kubwa lilikuwa linavuka mataa kwa kasi na kusababisha ajali mbaya iliyokatisha uhai wake; “Kulazimika kusimamia majukumu yote ya wazazi wawili nikiwa peke yangu.
“Imenifanya kuwa na nguvu zaidi na kunionyesha kuwa nina uwezo wa kufanya chochote lakini wakati huo huo nataka kupumua, nataka kwenda kwenye mahala pa kupumzika angalau mara moja bila watoto wadogo wakinifuata nyuma.
“Nataka niweze lala ndani, sihitaji kuamka kwa sababu watoto wameamka, nataka kupumzika na niko vizuri kusema hivyo sasa, kwa sababu mimi ni mwanadamu….” aliandika marehemu Olivia kwenye ukurasa wake wa Instagram kabla ya umauti kumkuta.
Social Plugin