Huku piramidi za Misri zikitambuliwa kote duniani, usanifu wa majengo ya Afrika umesalia kutojulikana-jambo ambalo wasanifu majengo Adil Dalbai na Livingstone Mukasa wanatumai litabadilika.
Wasanifu majengo hawa ni sehemu ya jopo lililochapisha muongozo wa usanifu wa majengo katika maeneo yaliyopo kusini mwa jangwa la sahara barani Afrika .Utafiti wao wa kina unajumuisha majengo yaliyojengwa kuanzia enzi za zamani, kipindi cha ukoloni-kama kituo kilichokarabatiwa hivi karibuni cha leri(hapo juu) katika mji mkuu wa Senegal, Dakar, mwaka 1910-na kuwa jengo la kisasa.
Haya ndio majengo 12 yaliyojengwa kwa ubunifu mkubwa zaidi, ya kihistoria na maarufu barani Afrika :
1) Kaburi la Kasubi, Uganda - 1882
Likiwa na ukubwa wa heka za ardhi ya kilimo katika mji mkuu wa Uganda , Kampala, eneo hilo la Kifalme la Kasubi ni maeneo wanapozikwa watu wa alme wa Baganda. Jengo hili lilijengwa kwa mbao zaidi na zana nyingine zitokanazo na mimea.
Eneo la ndani limetengenezwa kwa kulifananisha na msitu mtakatifu na paa lake lina pete 52 kila moja ikiwakilisha koo za watu wa kabila la Baganda.
Mukasa, ambaye alizaliwa Uganda, alitembelea makaburi kwa mara ya kwanza wakati alipokuwa na umri wa miaka 10 . "Lilikuwa ni la kushangaza,"aliiambia BBC. "Sio tu kwa ukubwa wake, bali mtindo mzima wa ujenzi wa jengo lenyewe.
"Lilijengwa mwishoni mwa karne ya 19 kabla ya kuanzioshwa kwa ujenzi wa kutumia zana za kisasa, kwa kutumia mbinu za kitamaduni
2) Soko la Lideta, Ethiopia - 2017
Likiwa na lango la kuingia lililojengwa kwa mtindo wa kisasa, soko hili lilijengwa katika mji mku wa Ethiopia, Addis Ababa, kwa matofali yenye uzito mdogo.
Ubunifu wake ulijumuisha vioo ambavyo vinathibiti kuingia kwa mwanaza asilia na kuingia kwa hewa ndani yake.
Zaidi ya hayo, kukatwa kwa vipande vya jengo hili na kurembeshwa kwa vigae vinavyong'aa ni mtindo wa vazi la kitamaduni la Ethiopia.
3) Hikma Complex, Niger - 2018
Muasisi wa kampuni ya ufanisi majengo ya Atelier Masōmī - raia wa Nigeria, Mariam Kamara, alirejesha msikiti wa zamani wa Hausa ambao ulikuwa umeporomoka, na kuongeza eneo la kijamii na maktaba.
Sehemu kubwa ya jengo hili imejengwa kwa matofali yaliyotengenezwa kwa udongo uliochimbwa takriban kilomita 5 (maili tatu ) katika kijiji cha Dandaji.
Kwa Dalbai, mradi .
"Ni wazi jengo lake la zamani ambalo lina mizizi ya utamaduni wa Kinigeria," msanifu majengo Mjerumani aliiambia BBC. " sio tu kitamaduni, lakini pia kiufundi kwasababu ujenzi wake ulitegemea mbinu za kitamaduni na zana."
4) Maropeng Visitors' Centre, Afrika Kusini - 2006
Likifahamika kama eneo la Cradle of Humankind World Heritage , Maropeng ni kituo cha wageni kilichojengwa wa usanii wa hali ya juu na limebuliwa kuwasaidia watu kujifunza kuhusu maendeleo ya awali ya binadamu wa sasa.
Jengo hili maarufu lilibuniwa na makampuni ya wasanifu majengo wa Afrika Kusini firms GAPP na MMA Studio.
Jengo lenyewe linafanana na mlima uliozikwa unaopanda juu ya ardhi, hilo linaonekana kweli kuwa kitu chenye uhusiano na asili.
5) Piramidi za Meroë, Sudan - 3,000BC
Usanifu wa zamani zaidi ulioingizwa katika mwongozo wa usanifu wa majengo ni piramidi hizi za Sudan zenye ngazi kila upande, ambazo zilijengwa miaka 3,000BC, zikiwa takriban kilomita 200 (maili 125 ) kutoka mji mkuu wa Sudan , Khartoum, katika Meroë kwenye bonde la mto Nile.
Eneo hili la urithi wa dunia la Unesco World Heritage wakati mmoja lilikuwa ni milki ya kale ya watu wa jamii ya Kushi na uvumbuzi julifichua mabaki ya mabafu ya kasri na ufalme.
Piramidi za eneo hili la makaburi lilijengwa kwa matofali ya mchanga.
6) Nyumba za Basotho, Lesotho - mwaka wa ujenzi haujulikani
Katika Lesotho, linafahamika kama pambo la "litema" . Jengo hili limejengwa kwa matofari ya udongo na plasta, na kupambwa kwa rangi za kitamaduni nyekundu ambayo ni alama ya damu ya uzazi na tambiko, rangi nyekundu inawakilisha usafi wa roho na amani , na rangi nyeusi inawakilisha mababu na ahadi ya mvua kwa "mawingi meusi ya mvua".
7) Maktaba ya Kenneth Dike , Nigeria - 1954
Maktaba hii mara kwa mara huelezewa kama kazi muhimu ya kile kinachofahamika kama "usasa wa maeneo ya joto ".
Lilijengwa wakati wa kipindi ambapo vioo vya jua vilipoanza kuwa maarufu, mchoro wa jengo hili ulibuniwa na Mfaransa mwenye asili ya Uswiss Le Corbusier ambaye alitumia "brise-soleil" -usanifu wa majengo unaopunguza joto ndani ya jengo kwa kuzuia mwangaza wa jua kuingia ndani.
Jengo hili lilibuniwa na Maxwell Fry na Jane Drew, ambao walikuwa waasisi wa vuguvugu la usasa katika England . Maktaba hii ni sehemu ya Chuo kikuu cha Ibadan - kilichoasisiwa na maafisa wa kikoloni wa Uingereza katika mwaka 1948
8) Great Mosque of Djenné, Mali - Karne ya 13
Mnara wa Uislamu, the Great Mosque ni jengu kubwa zaidi lililojengwa duniani. Msikiti huu ni ishara ya mji wa Djenné, uliostawi kama kituo cha biashara kati ya mwaka 800 na 1250.
Kukta laini za jengo hili zimejengwa kwa matofali yaliyochomwa kwa jua, na mchanga na plasta ya udongo.
9) Kasri la Himaya ya Fasilides, Ethiopia - mwanzoni mwa karne ya 17.
Kasri hili lipo katika mji wa kaskazini mwa Ethiopia wa Gondar, katika eneo lililopo katikati ya milima la "Fasil Ghebbi"
Eneo hilo linajumuisha baadhi ya kasri 20, majengo ya ufalme , makanisa yaliyopambwa, majengo ya kifalme na majengo ya kipekee.
Muundo wa majengo haya ulishawishiwa na mtindo ulioletwa na wa Gondarna wamishonari wa Kijesuit.
10) Chapel ya Dominican, Nigeria -1973
Msanii Demas Nwoko alichanganya ufundi wa ujenzi na usasa pamoja na mtindo wa ujenzi wa kitamaduni katika kanisa hili dogo la kidomonican katika Ibadan.
Jengo hili linajumuisha zana kama vile mbao na vyuma kwneye lango lake.
11) Msikiti mkubwa -Great Mosque, Benin - 1912-1935
Msikiti huu uliopo katika mji mkuu wa Benin, Port-Novo, ni mfano bora wa usanifu wa majengo unaochanganya mtindo wa Kiafrika na Kibrazili wa ujenzi wa makanisa ya kati ya karne 17 na 18 kaskazini -mashariki mwa jimbo la Brazili la Bahia. Rangi ya manjano inayong'ara, kahawia, kijani na blu ni kumbukumbu ya usanifu wa kihistoria wa Bahia.
Kwenye mwambao wa Along the West African coast, it is one of many Afro-Brazilian mosques built in the early 20th Century by returning descendants of freed slaves.
12) Mapungubwe Interpretation Centre, Afrika Kusini- 2009
Likiwa katika ardhi yenye miambak katikati ya mbuga ya taifa ya wanyama ya Mapungubwe, kituo hiki kilishinda tuzo ya usanifu ya Peter Rich ya mwaka 2009 ya Jengo la dunia la mwaka katika tamasha la dunia la usanifu -World Architecture Festival.
Mtindo wa jengo hili umejengwa kwa "mbinu iliyosahaulika kwa muda mrebu kutoka Afrika magharibi na kupelekwa katika Catalonia, na ambao ulikuwa ukitumiwa na wasanifu majengo kama vile Antoni Gaudi", kwa mujibu wa Rich.
Matofali ya matope yalitengenezwa kwa kutumia udongo kutoka katika maeneo ya ujenzi na ni 5% tu ya sementi ya nyongeza iliyotumiwa kutengeneza mchanganyiko wa udongo.
CHANZO - BBC SWAHILI
Social Plugin