Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MWANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE AUAWA KWA KUCHOMWA AKIGOMBANIA MWANAMKE BAA

Mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya upili ya Kapsinendet kaunti ya Bomet nchini Kenya amefariki dunia baada ya kudungwa kisu na mwanaume mmoja wakiwa kwenye baa wakigombania mwanamke.

Inaelezwa kwamba wawili hao walikuwa wakizozania mwanamke mmoja kwenye baa kabla ya mshukiwa kuchukua kisu na kumdunga mwanafunzi huyo.

Kwa mujibu wa taarifa za Citizen, mwanaume huyo ambaye hajatambulika anadaiwa kumdunga mwathiriwa kisu mara mbili kwenye shingo kabla ya kutoroka.

Mwanamke aliyekuwa akipiganiwa alitoroka eneo la tukio baada ya kushindwa kuwatuliza wanaume hao

Mwanamke huyo anasemekana alihamia eneo la Siongiroi kutoka Sotik hivi karibuni.

Maafisa wa polisi walifanikiwa kumkamaata mshukiwa na wanamzuilia katika kituo cha Chebunyo kaunti ya Bomet huku uchunguzi ukianzishwa.

Chanzo - Tuko News

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com