Kamanda wa Polisi mkoani Kagera Awadhi Juma Haji
Jeshi la Polisi mkoani Kagera linamshikilia Emmanuel Mdende (51) mkazi wa Kijiji cha Mugajwale, Tarafa ya Rubale wilaya ya Bukoba, kwa tuhuma za kumuua kwa kumkata kwa panga mke wake Odiria Lucas (47), akimtuhumu kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine.
Kamanda wa Polisi mkoani Kagera Awadhi Juma Haji, amesema kuwa tukio hilo limetokea Oktoba 11 mwaka huu saa 8:45 mchana, ambapo mtuhumiwa huyo alimkata mke wake shingoni mara nne kwa upande wa nyuma na kusababisha kifo chake papo hapo.
Kwa mujibu wa Kamanda huyo baada ya mtuhumiwa kukamatwa amekiri kuhusika na tukio hilo, na kutumia fursa hiyo kutoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi, na badala yake watumie vyombo vya sheria vilivyopo kumaliza matatizo yanayojitokeza katika jamii.
Chanzo - EATV
Social Plugin