Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NABII KATAPIA AKUTWA AMEFARIKI KWENYE GETI LA HOSPITALI ARUSHA



JESHI la Polisi mkoano Arusha limesema wanaendelea na uchunguzi wa kifo cha mtu aliyetambulika kama Mchungaji au Nabii Abraham Peter maarufu ‘KATAPIA‘ ambaye mwili wake umekutwa nje ya geti la Hospitali ya Mount Meru Arusha akiwa tayari ameshafariki huku akiwa amevuja damu nyingi kutokana na jeraha kubwa mguuni.

Kamanda wa Polisi Arusha, Justine Masejo amethibitisha na kusema…. “Taarifa tulizoambiwa ni kwamba alikuwa akifanya mahubiri katika madhehebu mbalimbali, siku ya tukio alijumuika na wenzake katika chakula cha jioni Arusha Mjini na walipoachana alipanda pikipiki ili kurudi sehemu alipofikia Sakina.

“Baadae Jeshi la Polisi tulipata taarifa ya kuonekana kwa mwili wa binadamu nje ya geti la Mount Meru, uchunguzi wa awali ulionesha alikua na jeraha mguu wa kushoto. Baada ya daktari kuufanyia uchunguzi mwili huo ilionekana kwamba chanzo cha kifo chake ni damu nyingi kuvuja kutokana na hilo jeraha la mguu wa kushoto.

“Jeraha wanasema limesababisha na kitu butu maana mguu haukuonekana kama umekatwa bali umevunjika. Tunaendelea kufatilia usafiri wa bodaboda alioutumia kwani iliita tu akapanda mara moja na kwanini alikua anakwenda Sakina lakini akakutwa Hospitali ya Mkoa, pia tunaendelea kuwahoji wale aliokua nao na watu wengine,” RPC Justine Masejo wa Arusha.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com