BENKI YA CRDB YACHANGIA NONDO KUSAIDIA UJENZI WA UKUTA SHULE KONGWE YA TOWN MJINI SHINYANGA...WADAU WAITWA


Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney (kulia) akimkabidhi nondo Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Town, Meshack Herman  (wa nne kushoto) kwa ajili ya ujenzi wa Uzio wa shule ya Msingi Town iliyoanzishwa mwaka 1942 Mjini Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney (kulia) akimkabidhi nondo kwa ajili ya ujenzi wa Uzio wa shule ya Msingi Town iliyoanzishwa mwaka 1942 Mjini Shinyanga.
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney (kulia) akimkabidhi nondo kwa ajili ya ujenzi wa Uzio wa shule ya Msingi Town iliyoanzishwa mwaka 1942 Mjini Shinyanga.
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney (kulia) akizungumza wakati akikabidhi nondo kwa ajili ya ujenzi wa Uzio wa shule ya Msingi Town iliyoanzishwa mwaka 1942 Mjini Shinyanga.
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Town, Meshack Herman (katikati) akiishukuru Benki ya CRDB kwa mchango nondo kwa ajili ya ujenzi wa Uzio wa shule ya Msingi Town iliyoanzishwa mwaka 1942 Mjini Shinyanga.


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Benki ya CRDB tawi la Shinyanga imechangia nondo 16 zenye thamani ya shilingi 400,000/= ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi yake katika ujenzi wa Uzio wa shule ya Msingi Town iliyoanzishwa mwaka 1942 Mjini Shinyanga.

Akizungumza wakati wa kukabidhi nondo hizo, leo Jumatatu Oktoba 4,2021 Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney amesema Benki hiyo iliahidi kuchangia nondo wakati wa Mahafali ya darasa saba yaliyofanyika Septemba 24,2021.

“Siku ya mahafali wakati wa harambee kuchangia ujenzi wa uzio/ukuta wa shule tuliahidi kuchangia nondo na leo katika awamu ya kwanza tumeleta nondo hizi 16 zenye thamani ya shilingi 400,000/=”,amesema Mneney.

Amesema nondo hizo zitakuwa chachu kwa wadau mbalimbali kujitokeza kufanikisha ujenzi wa uzio wa shule hiyo kongwe iliyopo katikati ya Mji wa Shinyanga lakini ipo wazi na kufanya wanafunzi kutokuwa salama.

Akipokea nondo hizo, Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Town, Meshack Herman ameishukuru Benki ya CRDB kwa mchango huo huku akiwaomba wadau mbalimbali waliosoma katika shule hiyo kusaidia ujenzi wa ukuta huo ili wanafunzi wawe salama kwani pako wazi hali inayosababisha watu wasio wema kupita katika shule hiyo na wakati mwingine kuwafanyia ukatili wa kijinsia wanafunzi.

“Tunawashukuru Benki ya CRDB kwa kutuunga mkono, bado tunahitaji vifaa vya ujenzi, mkipata naomba mtuletee. Hivi sasa tunaendelea na zoezi la kukusanya vifaa vya ujenzi kutoka wadau,tunaomba wadau wajitokeze kufanikisha ujenzi wa ukuta wenye urefu wa mita 500 na urefu wa kozi 6”,amesema Herman.

Kwa mdau yeyote anayependa kuchangia ujenzi wa ukuta wa shule ya Msingi Town yenye jumla ya wanafunzi 1165 (wasichana 647,wavulana 518) iliyopo Mjini Shinyanga afike shuleni au awasiliane na Mwalimu Mkuu Meshack Herman kwa simu namba 0716457448



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post