Picha ya mkazi wa Srbac, Vokin Kusic
Mzee wa miaka 72 mkazi wa Srbac, nchini Bosnia anayejulikana kama Vokin Kusic ametumia zaidi ya miaka sita kukamilisha ujenzi wa nyumba ya kipekee yenye matairi inayozunguka baada ya kuchoshwa na malalamiko ya mkewe.
Kusic ameeleza kuwa aliamua kufanya hivyo baada ya mke wake kuzidisha malalamiko ambapo inadaiwa kuwa alikuwa anahitaji nyumba yenye muonekano tofauti zaidi ili awe na uwezo wa kuona kuchomoza kwa jua wakati huo huo na wapita njia katika eneo hilo.
Nyumba inaweza kuzunguka na kukamilisha mzunguko wa duara kwa saa 24 kama speed yake ni ndogo (slowest speed), lakini ikizungushwa kwa speed zaidi inaweza kutumia sekunde 22 pekee.
Social Plugin