Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA AWAONYA WANAOTAKA KUJUA RANGI YAKE HALISI



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaonya viongozi wa ngazi mbalimbali kuanzia Mawaziri hadi Wakurugenzi kutumia vizuri fedha za mkopo jumla ya Shilingi Trilioni 1.3 kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF).

Onyo hilo amelitoa leo Jumapili Oktoba 10, 2021 wakati akihutubia taifa kupitia uzinduzi wa Kampeni ya Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko-19 kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre jijini Dodoma.

''Kwa wale wanaotaka kuzijua rangi zangu halisi, mkinitazama hivi mnasema Mhe. Rais ni mweupe lakini nina rangi halisi, kwa hiyo wanaotaka kuzijua rangi zangu halisi wajaribu kudokoa pesa hizi au wabadilishe matumizi ya fedha hizi bila maelewano,''amesema Rais Samia.

Via>> EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com