TASAF WAIDHINISHA SHILINGI BILION5.5 KUNUSURU KAYA MASIKINI ZILIZOATHIRIKA NA UVIKO 19

 
Na Magrethy Katengu - Dar es salaam
Mfuko wa Maendeleo ya jamii TASAF umeidhinisha shilingi bilioni 5.5 kwa ajili ya kuondoa athari za kiuchumi zilizochochewa na mlipuko wa UVIKO-19 kwa kaya walengwa 40,740 kwa kuwaondolea umaskini wa kipato kwa kuwapatia ruzuku za kujikimu,ajira za muda na kuwaongezea ujuzi,maarifa na elimu ya ujasiriamali.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati akieleza utekelezaji wa mpango maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya uviko-19 ,Mkurugenzi mtendaji wa TASAF ,Ladislaus Mwamanga amesema kupitia fedha hizo kaya walengwa 40,740 wenye uwezo wa kufanya kazi ambao wanaishi katika maeneo ya mijini,watafanyakazi katika miradi ya jamii na kulipwa ujira wa wastani wa shilingi 135,000/= kwa mwezi.

"Usimamizi utafanyika kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa viwango kulingana na thamani ya fedha,ni matumaini yeti kwamba fedha hii iliyotengwa kwaajil ya TASAF itasisimua uchumi wa kaya uliokuwa umedorora kutokana na athari za UVIKO-19 na hivyo kuchangia katika mapambano ya kuondoa umasikini ambayo no sehemu ya mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa", amesema Mwamanga.

Aidha amesema serikali inaendelea kutekeleza mipango na mikakati mbalimbali katika kupunguza umaskini wa Watanzania wanaoishi katika mazingira duni na inafanya jitihada kubwa kupata fedha kutoka vya ndani,mikopo na misaada kutoka kwa wadau wa maendeleo.

Hata hivyo amesema mara baada ya uzinduzi wa kipindi cha pili cha awamu ya tatu   TASAF nchi ilipata janga la Uviko 19 na kubainisha shughuli nyingi kusimama ili kuzuia maambukizi kwa njia ya mikusanyiko hivyo walengwa hawakupata fursa ya kukutana wao kwa wao kwa wao na kubadilishana uzoefu.

TASAF inatekeleza mpango wa kunusuru kaya za walengwa katika halmashauri 184 za tanzania bara,unguja na pemba zenye idadi ya takribani kaya milion 1.4 zenye watu wanaokadiriwa kufkikia milioni 10.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post