Kutokea pande za Texas Marekani, tuna habari mnyama aina ya Tiger aliyepewa jina la Elsa ambaye amefanyiwa sherehe ya Birthday kwa kutimiza mwaka mmoja tangu aokotwe na kulelewa katika hifadhi ya wanyama pori ya Black Beauty Ranch iliyopo Texas.
Elsa aliokotwa wakati wa baridi kali akiwa amefungiwa katika kibanda ambacho kilionekana kama jela kwake kutokana na udogo wa kibanda hicho, mamlaka zinazohusika na wanyama pori nchini humo zilimuondoa Elsa kwenye karaha hiyo baada ya majirani kutoa taarifa juu ya uwepo wa Tiger ambaye anateseka na baridi maeneo ya San Antonio.
Elsa alikutwa akiwa amejichubua ngozi yake na sehemu kadhaa za mwili wake hakukuwepo na manyoya kutokana na kujikwaruza katika kibanda hicho kidogo. Elsa sasa amekuwa na afya njema huku akiwa na uzito wa 83 Kg. Katika sherehe hiyo Tiger huyo (Elsa) aliwekewa vyakula mbalimbali pamoja na vitu vya kuchezea!
Social Plugin