WAZIRI MHAGAMA ATOA MAELEKEZO KWA KAMATI ELEKEZI YA ULINZI WA WANAWAKE NA WATOTO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Masuala ya  Sera, Uratibu  Bunge, Kazi,  Vijana , Ajira na Watu wenye Ulemavu  Mhe. Jenista Mhagama 

Na Jackline Lolah Minja -Morogoro

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Masuala ya  Sera, Uratibu  Bunge, Kazi,  Vijana , Ajira na Watu wenye Ulemavu  Mhe. Jenista Mhagama ameilekeza kamati elekezi ya ulinzi wa wanawake na watoto kusimamia na kuandaa mikakati madhubuti itakayosiadia kiumarisha utendaji wa kamati hiyo kwenye ngazi zote na kuhakikisha rasilimali fedha kwaajili ya utekelezaji wa afua za MTAKUWWA zinatengwa nakutolewa kwenye wizara na taasisi husika ili kuendelea kubaini kada zenye upungufu mkubwa wa  watendaji hususani katika ngazi ya kata na vijiji.

Akifungua kikao cha kamati elekezi ya ulinzi wa wanawake na watoto kilichofanyika mkoani Morogoro na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, Mhagama amesema katika kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto hapa nchini serikali kwa kushirikiana na wadau imewezesha uwanzishwaji wa madawati ya jinsia na watoto katika vituo vya polisi.

“Ndugu washiriki hadi kufikia mwaka 2020/2021 jumla ya madawati 420 yameanzishwa katika vituo mbalimbali vya polisi hapa nchini aidha jitihada za kukabiliana na vitendo vya ukatili katika vyuo vya elimu ya juu na kati zimeendelea ambapo hadi kufikia februari 2021 jumla ya madawati matano ya jinsia yameanzishwa katika taasisi za elimu ya juu na kati”, amesema.

Aidha Mhagama amesema ukatili dhidi ya wanawake unabaki kuwa changamoto na kizuizi cha jitihada za kuelekea usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake hivyo zinahitajik jitihada endelevu za pamoja baina ya serikali na wadau.

“Nafahamu MTAKUWWA unalengo la kupunguza ukatili kwa wanawake na watoto kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2021/22 ili kufikia lengo hilo serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imekuwa ikitekeleza afua mbalimbali zinazolenga kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kupitia maeneo nane ya utekelezaji”,amesema.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Masuala ya  Sera, Uratibu  Bunge, Kazi,  Vijana , Ajira na Watu wenye Ulemavu  Mhe. Jenista Mhagama 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post