Kampuni ya Madini ya Barrick, imedhamini wajasiariamali 100 wanaoishi vijiji jirani na mgodi wa Bulyanhulu kushiriki katika maonyesho ya wajasiariamali yaliyoandaliwa na taasisi ya Kangaroo na kufanyika mkoani Shinyanga.
Katika maonyesho hayo ya wiki moja yaliyomalizika mwishoni mwa wiki, wajasiarimali kutoka mikoa yaKanda ya ziwa walipata fursa ya kuonyesha bidhaa zao, kupatiwa mafunzo pia kampuni mbalimbali zilishiriki kwenye maonyesho haya ambayo yamevutia wanachi wengi sambama na kutembelewa na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Barrick kupitia sera yake ya kusaidia huduma za kijamii (CSR), imekuwa na programu za kuwezesha wajasiarimali wanaoishi jirani na maeneo yake ya kazi sambamba na kufanikisha miradi ya kijamii hususani katika sekta ya afya ,elimu na ujenzi wa miundombinu ya barabara.
Wageni mbalimbali wakitembelea banda ya Barrick na wajasiriamali pia maofisa Waandamizi wa Barrick walitembelea mabanda ya wajasiriamali
Social Plugin