Mwanamke mmoja amejifungua watoto saba mjini Abbottabad huko Pakistan.
"Mungu ametujaalia watoto wanne wa kiume na watatu wa kike. Tunafuraha sana."Alisema mume wake,Yar Mohammad
Bw. Mohammed anasema uchunguzi wa awali ulipobaini mke wake amebeba watoto kadhaa tumboni walishauriwa waende hospitali kuu kwa uangaalizi wa karibu.
Madaktari waliomhudumia walishangazwa sana na hali ya mwanamke huyo.
Kulingana na Dkt Hina Fayaz, daktari bingwa wa wanawake katika Hospitali ya Jinnah huko Abbottabad, mwanamke huyo alikuja kwake kwa mara ya kwanza Jumamosi.
Anasema, "Baada ya uchunguzi wa ultrasound na ripoti zingine, tuligundua kuwa ana watoto watano ndani ya tumbo lake na ujauzito wake ulikua zaidi ya miezi minane"
Dk Hina Fayaz anasema kwamba alishtuka sana kuona ripoti ya matibabu ya mwanamke huyo.
Madaktari waliomhudumia walishangazwa sana na hali ya mwanamke huyo.
"Alikuwa na shinikizo la damu iliyotajwa kuwa ya kiwango hatari. Tumbo lake lilikuwa limevimba. Kabla ya hapo, alikuwa amejifungua na watoto wawili kwa nja ya upasuaji. Alikuwa na maumivu makali kwenye kovu la upasuaji wa kwanza.''
Hata hivyo madaktari walifanikiwa kuwatenganisha watoto hao kabla ya kuwatoa tumboni.
"Tulijitahidi sana kuhakikisha mama asipoteze damu nyingi wakati wa kuwatenganisha."
Watoto hao kwa sasa wanapewa uangalizi maalum.
Baba yao anasema kuwatunza haitakuwa kazi ngumu kwa sababu anaishi na jamaa zake.
CHANZO - BBC SWAHILI