Akizungumza kwenye maadhimisho hayo, Dk. Sengati amewahakikishia wazee mkoani Shinyanga, kuwa Serikali itaendelea kutatua changamoto zao mbalimbali, ikiwamo kuboresha huduma za Afya, na kuwapatia kadi za matibabu bure zikiwamo na Bima za Afya CHF iliyoboreshwa.
Alisema Serikali inatambua mchango mkubwa wa wazee hapa nchini, katika kuchota busara zao, hekima, na hata kudumisha amani ya nchi, na pia kuliletea Taifa maendeleo, hivyo hawana budi kuendelea kuwalinda pamoja na kuwapatia huduma bora.
"Serikali tutaendelea kutenga madirisha ya wazee kwenye huduma zetu za afya, upatikanaji wa madawa ya magonjwa ya wazee, kuwapatia kadi za matibabu bure, na bima za afya CHF, naahidi kutoa Sh.500,000 kwa ajili ya kuongeza idadi ya wazee kukatiwa bima ya CHF, ambapo kwa sasa wapo 5,571, na wenye kadi bure wapo 21,000 na tunajumla ya wazee 66,000,”alisema Dk. Sengati.
“Pia naagiza kila Halmashauri mkoani Shinyanga, kuhuisha Mabaraza ya wazee na kuyasimamia, kutenga bajeti na kuyawezesha katika shughuli zao mbalimbali, sababu wazee hawa ni hazina yetu katika Taifa hivyo lazima tuwahudumie pamoja na kuwalinda,”aliongeza.
Katika hatua nyingine Dk. Sengati, aliwataka Wazee wajitokeze kwa wingi kupata Chanjo ya UVIKO-19 Sanjari na wananchi, na kupuuza maneno ya upotoshwaji juu ya chanjo hiyo, huku akionya wale ambapo watabainika kufanya upotoshaji mkoani Shinyanga watachukuliwa hatua kali.
Kwa upande wake, Katibu wa Baraza la Wazee mkoani Shinyanga Anderson Lyimo, akisoma Taarifa ya Wazee mkoani humo, ameipongeza Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassani, kwa kuendelea kutatua changamo zinazowakabili wazee, likiwamo suala la matibabu bure pamoja na kutolipa Kodi ya Majengo.
Aidha, alisema licha ya Serikali kuendelea kutatua changamoto hizo za Wazee, bado wanakabiliwa na tatizo la uhaba wa madawa ya wazee kwenye huduma za kiafya, kutekelezwa na watoto wao, huku wakiomba pia nao waingizwe kwenye upewaji wa mikopo ya Halmashauri asilimia 10, ili wajikwamue kiuchumi kwa kufanya shughuli mbalimbali za kiujasiriamali.
Naye Mratibu wa Shirika la TAWLAE ambalo linatetea haki za Wazee mkoani Shinyanga Eliasenya Nnko, ameipongeza Serikali kuendelea kutatua changamoto za wazee, pamoja na kupunguza tatizo la mauaji ya wazee ya kukatwa mapanga sababu ya imani potofu za kishirikina.
Pia Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Yudas Ndungile, alisema Serikali itaendelea kuboresha huduma za afya kwa wazee, huku akitaja Takwimu za watu ambao mpaka sasa wameshapata Chanjo ya UVIKO -19 kuwa ni 10,000 kati ya Dozi 25,000 ambayo ilitolewa na Wizara ya Afya, na kubainisha kuwa zoezi linaendelea vizuri la utoaji Chanjo hiyo ambapo kila siku wanachanja wananchi 1,200.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Philemon Sengati akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya Wazee Duniani yaliyofanyika mkoani humo katika Kijiji cha Nyandekwa Manispaa ya Kahama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Philemon Sengati, akihamasisha Wazee pamoja na Wananchi kujitokeza kwa wingi kupata Chanjo ya UVIKO-19 ili siku wakipata maambukizi ya virusi vya Corona itawasaidia kuokoa maisha yao.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Zuwena Omary, akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya Siku ya Wazee.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Yudas Ndugile, akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya siku ya Wazee.
Mwenyekiti wa baraza la wazee la Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Ziporah Pangani, akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mabala Mlolwa kwenye maadhimisho hayo ya siku ya Wazee.
Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini Jumanne Kishimba, akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya siku ya Wazee.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Festo Kiswaga, akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya siku ya Wazee.
Katibu wa Baraza la Wazee mkoani Shinyanga Anderson Lyimo, akisoma taarifa ya Wazee kwenye maadhimisho ya siku ya Wazee.
Mratibu wa Shirika la kutetea haki za Wazee (TAWLAE) Eliasenya Nnko, akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya Wazee.
Wazee mkoani Shinyanga wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani, yaliyofanyika kimkoa katika Kijiji cha Nyandekwa Manispaa ya Kahama.

Wadau wa Masuala ya Wazee kutoka Shirika la TAWLAE, wakiwa kwenye Maadhimisho ya siku ya Wazee.
Wazee mkoani Shinyanga wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani, yaliyofanyika kimkoa katika Kijiji cha Nyandekwa Manispaa ya Kahama.
Viongozi mkoani Shinyanga wakiwa wameketi Meza kuu kwenye Maadhimisho ya siku ya Wazee Duniani, yaliyofanyika kimkoa katika Kijiji cha Nyandekwa Manispaa ya Kahama, katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Philemon Sengati, kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee mkoani Shinyanga Faustine Sengerema, na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga.
Viongozi wa Serikali pamoja na wadau wa Masuala ya Wazee wakiwa kwenye Maadhimisho ya siku ya Wazee katika Kijiji cha Nyandekwa Manispaa ya Kahama.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Philemon Sengati, mwenye Tishet ya Njano, akihamasisha Wazee kupata Chanjo ya UVIKO-19 kwa hiari yao kwenye mabanda ambayo yamewekwa, sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wazee.ikipata chanjo hiyo ni Mzee Maria Masanja na anayempatia Chanjo hiyo ni Mratibu wa Elimu Afya kwa Umma wilayani Kahama Asteria Kamanga.
Mzee Juma Ntale, akipata Chanjo ya UVIKO-19 kwa hiari yake mwenyewe kwenye maadhimisho ya siku ya Wazee, akimpatia chanjo hiyo ni Afisa Muuguzi kutoka Hospitali ya wilaya ya Kahama Abdala God.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk, Philemon Sengati, kulia akimpatia Kadi ya Bima ya CHF iliyoboreshwa Mzee Sofia Katunda kwenye Madhimisho hayo ya siku ya Wazee.
Zoezi la utoaji kadi Bima za Afya CHF likiendelea.
Zoezi la utoaji kadi ya Bima za Afya CHF likiendelea.
Zoezi la utoaji kadi Bima za Afya CHF likiendelea.
Wazee wakishindana kuvua Kamba kwenye Maadhimisho hayo ya siku ya Wazee Duniani.
Wazee wakishindana kuvua Kamba kwenye Maadhimisho hayo ya siku ya Wazee Duniani.
Wazee wakishindana kukimbiza kuku kwenye Maadhimisho hayo ya siku ya Wazee Duniani.
Wazee wakishindana kukimbiza kuku kwenye Maadhimisho hayo ya siku ya Wazee Duniani.
Wazee wakiwa katika Maandamano huku wakionyesha Bango lenye ujumbe wa Maadhimisho ya siku ya Wazee Duniani.
Na Marco Maduhu- Shinyanga
Social Plugin