Picha ya mwanzilishi na Mkurugenzi mtendaji wa Facebook, Instagram na WhatsApp
**
Baada ya mitandao ya kijamii ya Facebook, Instagram na WhatsApp kutofanya kazi kwa saa kadhaa inaelezwa kuwa utajiri wa mwanzilishi na Mkurugenzi mtendaji wa mitandao hiyo.
Mark Zuckerberg umeshuka kwa wastani wa dola Bilioni 5.9 hadi 7 zaidi ya Trilioni 13 kwenye saa 6 ambazo ili-stuck.
Facebook, Instagram na WhatsApp ilipata matatizo ya kimtandao na kutofanya kazi kutokana na kufeli kwa mabadiliko ya mfumo na sio udukuzi kutoka nje ya kampuni ambapo imesababisha Mark kushuka mpaka nafasi ya 6 kwenye orodha ya matajiri Ulimwenguni akiwa na utajiri wa dola azidi ya Bilioni 116 kwa mujibu wa Forbes.
Tayari Huduma za mitandao ya kijamii ya Facebook, WhatsApp na Instagram zimerejea tena kwa watumiaji wake kama kawaida baada ya kukatika kwa takribani saa sita huku Kampuni hiyo ikisema sababu ilikuwa ni kufeli kwa mabadiliko ya mfumo duniani kote.
Huduma zote tatu zinamilikiwa na Kampuni ya Facebook na hazikuweza kupatikana kwenye wavuti au kwenye programu za simu za mkononi kuanzia majira ya saa 1 jioni ya jana Oktoba 4, 2021.
Downdetector, ambayo inafuatilia kukatika kwa huduma za mitandao ya kijamii ilisema ni hitilafu kubwa zaidi kuwahi kutokea, na ripoti milioni 10,6 za matatizo kutoka kwa wateja kote ulimwenguni.
Katika taarifa Jumanne, Facebook ilisema kuwa mabadiliko mabaya ya usanidi yaliathiri mifumo ya ndani ya kampuni ambayo ilikuwa vigumu kujaribu kusuluhisha tatizo hilo. Iliongeza kuwa hakuna ushahidi kwamba data ya watumiaji imeathiriwa kutokana na wakati huu kukatika kwa huduma.
Siku ya Jumatatu, Facebook ilituma ujumbe wa kuwaomba msamaha kwa wale walioathiriwa na kukatika kwa huduma zake.
Watu wengine pia waliripoti shida kutumia huduma nyingine zinazotegemea Facebook kama Oculus, na programu ambazo zinahitaji kuingia kwa Facebook ziliathiriwa, pamoja na Pokémon Go.
Kukatika kwa kiwango hicho kwa muda mrefu ni nadra. Usumbufu mnamo 2019 uliacha Facebook na programu zake zingine kutoweza kufikiwa kote ulimwenguni kwa zaidi ya masaa 14.
Usumbufu huo unakuja siku moja baada ya mahojiano na mfanyakazi wa zamani wa Facebook ambaye alivuja nyaraka kuhusu kampuni hiyo. Frances Haugen aliliambia shirika la habari la CBS Jumapili kwamba kampuni hiyo ilikuwa imeweka kipaumbele kuhusu kuboresha masuala ya usalama.
Siku ya Jumanne atatoa ushahidi mbele ya kamati ndogo ya Seneti katika kikao kinachoitwa “Kulinda Watoto Mitandaoni”, juu ya utafiti wa kampuni hiyo juu ya athari ya Instagram kwa afya ya akili ya watumiaji wachanga.
Social Plugin