Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

YANGA YAZIDI KUNG'AA, YAICHAPA AZAM FC 2 - 0 KWA MKAPA

 

Na Emmanuel Mbatilo Dar es salaam

Klabu ya Yanga imeendeleza ubabe katika Ligi ya NBC mara baada ya leo kuichapa Azam Fc mabao 2-0 kwenye dimba la Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.

Mechi hiyo  ambayo ilikuwa ya aina yake hasa Yanga kucheza kandanda safi pale katika ambapo walipatawala kuanzia mpira  ulivyoanza mpaka dakika 90.

Yanga ilianza kupata bao dakika ya 35 kupitia kwa mshambuliaji wao mahili kutoka nchini Kongo Fiston Mayele ambaye aliunganisha mpira ambao ulipigwa na Kibwana Shomari.

Yanga ilikwenda mapumziko ikiwa inaongoza kwa bao 1-0 huku mashabiki uwanjani wakionekana wakihitaji ushindi wa mabao mengine katika mechi hiyo.

Kipindi cha pili kilianza huku Yanga ikiendelea kutawala mchezo hasa kutengeneza nafasi nyingi za wazi bila mafanikio.

Dakika 73 ya mchezo winga raia wa Jamhuri ya Kongo Jesus Moloko aliipatia klabu yake bao la pili na kufanya matokeo kuwa 2-0 Yanga ikaondoka na pointi tatu muhimu kwenye mchezo huo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com