BANDARI TANGA YAKUTANA NA WADAU MKOA KILIMANJARO


MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro  Stephen Kagaigai akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wa Bandari Mkoani humo
AFISA Uhusiano wa Bandari ya Tanga Adam akizungumza wakati wa kikao hicho
KAIMU Meneja wa Bandari ya Tanga Donald Ngaire kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Stephen Kigaigai wakifuatilia kikao hicho.


BANDARI ya Tanga imekutana na na wadau wa Bandari Mkoa wa Kilimanjaro mkoani Kilimanjaro lengo likiwa kuelezea fursa zilizopo kwenye Bandari hiyo huku wakiwaomba kuitumia kupitisha shehena zao  kutokana na mabadiliko makubwa ya uwekezaji yaliyofanywa na Serikali ikiwemo uboreshwaji wa miundombinu

Mkutano huo umefanyika Octoba 20 mwaka huu ambapo wadau walipata fursa ya kuweza kujadili masuala mbalimbali na hatimaye kuweza uhitaji wao wa kutaka kutumia Bandari ya Tanga 

Mabadiliko hayo ni miongoni mwa maboresho ambayo yameiwezesha Bandari hiyo kuongeza wigo mpaka wa kuhudumia shehena inayoshuka ikiwemo kuongezeka kina cha maji na ujenzi wa gati hatua ambayo imesaidia kuondosha changamoto zilizokuwepo awali.

Kikao hicho ambacho Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Donald Ngaire aliwaambie wadau hao kwamba wakitumia bandari hiyo itakuwa ni rahisi kwao kuweza kutoa mizigo yao kwa muda mchache kutokana na maboresho makubwa yaliyofanyika ambayo yamelenga kufungua fursa za huduma.

"Lengo kubwa ni  kuwajulisha mabadiliko makubwa ya uwekezaji ikiwemo kuongeza kina cha maji na Ujenzi wa gati na Mkutano huo umeongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh Stephen Kagaigai ,Kaimu Meneja wa Bandari Donald Ngaire na Idara ya Masoko na Uhusiano.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post