MWENYEKITI wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) Brigedia Jenerali Mstaafu Aloyce Mwanjile akizungumza jambo wakati wa kikao cha wadau wa Korosho Mkoa wa Tanga kilichofanyika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga |
MWENYEKITI wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) Brigedia Jenerali Mstaafu Aloyce Mwanjile |
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho |
MKURUGENZI wa Tari Naliendele akisisitiza jambo wakati wa kika hicho |
KATIBU Tawala Msaidizi -Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Tanga ,Mhandisi Emigidius Kasunzu akitoa wasilisho la Utekelezaji wa Shughuli za Korosho katika Mkoa (Changamoto na mafanikio). |
MENEJA wa Benki ya NMB Tawi Madaraka Jijini Tanga Elizaberth Chawinga akichangia jambo kwenye kikao hicho
MKUU wa wilaya ya Korogwe Basila Mwanukuzi katika akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo wakati wa kikao hicho kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani
MENEJA wa Bodi ya Korosho Mkoa wa Tanga Ugumba Kilasa kushoto akifuatia kwa umakini kikao hicho wa kwanza kulia ni Afisa Kilimo wa Bodi ya Korosho Tanzania Tawi la Tanga Frank Mfutakamba
Wadau wa zao la Korosho wakifuatilia kikao hichoWAWEKEZAJI wa Zao la Korosho wakifuatilia kikao hicho kwa umakini
NA OSCAR ASSENGA,TANGA.
MWENYEKITI wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) Brigedia Jenerali Mstaafu Aloyce Mwanjile amesema bodi hiyo kwa kushirikiana na Tari Naliendele wanatarajia kuajiri maafisa ugani waliosomea zao hilo kila wilaya inayolima zao hilo ambao watasaidia kuinua kiwango cha uzalishaji na hari kwa wakulima.
Aliyasema hayo Jijini Tanga wakati wa kikao cha wadau wa Korosho wa Mkoa wa Tanga katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambapo alisema watafanya hivyo ili kuhakikisha kilimo chga zao hilo kinakuwa na tija kubwa kuliko ilivyokuwa hapo awali ikiwemo kuongezeka kwa uzalishaji.
Alisema sambamba na hilo bodi kwa kushirikiana na Taasisi ya Tari Naliendele watatoa elimu maeno yote kutokana na kwamba wamegundua maafisa ugani wengi hawajakijikita kwenye za la Korosho na hivyo kupelekea wakulima kushindwa kuwapa ushauri mzuri wakulima .
"Kwa kuliona hili ndio maana bodi inakusudia kuaajiri maafisa ugani waliosomea korosho na watakuwepo kila wilaya inayolima korosho na watasaidia kuinua kiwango cha uboreshaji wa zao na wakulima kwa kulima kilimo chenye tija na mafanikio makubwa"Alisema
Mwenyekiti huyo alisema kwa sasa bodi hiyo inawahakikishia wakulima wa zao la korosho mkoa wa Tanga na Tanzania wanayo mikakati ya kuhakikisha zao hilo liunaendeezwa kwa kuhakikisha uzalishaji unaongezeka na kwa kuanza bodi itatoa miche au mbegu za kutosha msimu unaokuja wa 2022/2023.
Alisema Korosho ni moja ya zao ambalo linaliingizia nchi fedha nyingi hivyo lazima kila mtu kwa nafasi yake aone namna gani ya kuhakikisha uzalishaji wa zao hilo unaongezeka na wenye tija kubwa.
Hata hivyo alisema hadi sasa halmashauri zote zinazolima korosho wameshawa andikia wapeleke mahitaji yao ya mbegu na wiki ijayo watakwenda kukaa kuona mahitaji hayo hiyo.
"Ombi langu Wakurugenzi na Wakuu wa wilaya msimamie ikiwezekana mtengeneze sheria ndogo ndogo zitakazo hamasisha watu kuanza mashamba ili kuzalisha korosha bora na zenye kiwango kizuri"Alisema
Aliongeza kwamba katika msimu 2022/2022 bodi ya Korosho kwa Kushirikiana na Wizara ya Kilimo wameandaa ununuzi wa viwatilifu ambavyo vitafika miko yote inayolima korosho hivyo wakulima hawana sababu ya kutokuzalisha korosho bora .
"Lakini pia kutatoa elimu ya upuliziaji wa viwatilifu ili kiwango cha Uzalishaji kiweze kuongezeka na kupanda na hivyo kusaidia kupunguza umaskini kwenye familia na kuongeza pato bado pia elimu ya ubanguaji inahitaji hususani kwa mkoa wa Tanga hivyo tutaona namna ya kuiandaa"Alisema Mwenyekiti wa Bodi Brigedia Mstaafu Aloyce.
Awali akizungumza kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima aliwaagiza Maafisa Kilimo wakafanye tathimini ya juu ulimaji wa Korosho na maeneo yao ili wajue kutokana na kwamba watakapohitaji kufanya mapinduzi ya uzalishaji wa zao hilo lazima wajue eneo ambalo linalimwa Korosho.