Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Singida Eva Mosha kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa Dk. Dorothy Mwaluko akizungumza katika maadhimisho hayo, ambapo pamoja na mambo mengine, alipongeza hatua ya shirika hilo ya kuandaa mashindano mbalimbali kwa wanafunzi, ikiwemo ya uandishi wa Insha na barua ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakisaidia kupanua fikra na kutoa mwanga katika kuchagiza ongezeko la ufaulu.
Kaimu Meneja wa Posta Singida Mary Kimaro akielezea namna shirika hilo lilivyofanya maboresho makubwa ya huduma zake mbalimbali za kidijitali, ikiwemo huduma mpya ya ‘Posta Kiganjani’ ambayo hutoa fursa kwa mteja kumiliki na kupata taarifa zote za sanduku lako la barua kupitia simu yako ya mkononi, sambamba na huduma ya ‘Duka Mtandao’ ambayo hutoa fursa kwa wafanyabishara, wajasiriamali na wabunifu mbalimbali kuuza na kutangaza bidhaa, ubunifu na mengine mengi kupitia huduma hiyo ya kidijitali popote pale ndani na nje ya nchi.
01. Mmoja Waataalamu wa Afya akitoa elimu juu ya Ugonjwa wa Uvico 19 kwenye sherehe za kilele cha maadhimisho ya Siku ya Posta mkoani Singida jana, sambamba na kuhamasisha wananchi kujitokeza na kupata chanjo ya ugonjwa huo ambayo ni salama katika kujilinda dhidi ya athari za ugonjwa huo.
01. Afisa wa Posta Singida Hadija Hamis akigawa vipeperushi vya elimu kwa umma kuhusiana na huduma mbalimbali za kidijitali zinazoendelea kutolewa ndani ya shirika hilo wakati wa sherehe za maadhimisho hayo jana
01. Afisa wa Posta Singida Nuru Malela akigawa vipeperushi vya elimu kwa umma kuhusiana na huduma mbalimbali za kidijitali zinazoendelea kutolewa ndani ya shirika hilo wakati wa sherehe za maadhimisho hayo jana
01. Afisa wa Posta Singida Erick Kiowi akigawa vipeperushi vya elimu kwa umma kuhusiana na huduma mbalimbali za kidijitali zinazoendelea kutolewa ndani ya shirika hilo wakati wa sherehe za maadhimisho hayo jana.
01. Afisa wa Posta Rehema Nchimbi akishiriki kikamilifu kwenye tukio hilo
01. Mwonekano wa zawadi mbalimbali zilizoandaliwa na shirika hilo kwa ajili ya washindi
Wafanyakazi wa Posta wakijiandaa kutoa zawadi kwa washindi.Mkuu wa Shule ya Sekondari Singitu, Masumbuko Makoye akipokea vifaa mbalimbali vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Covid 19 vilivyotolewa na Shirika la Posta Singida kama mwendelezo wa kuunga mkono juhudi mbalimbali zinazotolewa na serikali katika kukabiliana na ugonjwa huo.
01. Mmoja wa wanafunzi akipokea zawadi
Mmoja wa wanafunzi akipokea zawadi kutoka Shirika la Posta Singida01. Shamrashamra zikiendelea
01. Shamrashamra zikiendelea
01. Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Posta Singida wakiwa kwenye picha ya pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria tukio hilo
01. Baadhi ya wanafunzi walioshiriki shindano la Shirika la Posta na kuibuka washindi wa shindano hilo kutoka Shule ya Sekondari Singitu iliyopo Kata ya Mtinko, Tarafa ya Mtinko, Wilaya ya Singida mkoani hapa wakiwa kwenye picha ya pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria tukio hilo pamoja na zawadi zao.
01. Baadhi ya wanafunzi wengine wa shule hiyo wakifuatilia maadhimisho hayo
Shamrashamra zikiendelea
01. Diwani wa Kata ya Mtinko Singida, eneo ilipo shule hiyo, Bilal Yusuph akizungumza kwenye maadhimisho hayo. Hata hivyo Diwani huyo aliomba Shirika la Posta kuangalia uwezekano wa kujenga darasa moja ndani ya shule hiyo litakalopewa jina la ‘Posta’ ili kusaidia kutatua changamoto ya miundombinu ya elimu ambayo ni kikwazo katika ustawi wa taaluma shuleni hapo.
Social Plugin