WASWAHILI wanasema Mungu sio hapangiwi….! Huu ni miongoni mwa misemo maarufu ya kiswahili inayotumiwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa jambo ambalo lilionekana kutowezekana kisha kuwezekana.
Ni takribani miezi nane iliyopita, hadithi ya kijana Nsanzimana Elie mwenye umri wa miaka 21, kutoka kusini mwa Rwanda ilipeperushwa na kituo cha Afrimax, na kusambaa karibu Dunia nzima.
Nsanzimana kijana aliyekuwa akiishi msituni na kutokana na muonekano wa sura yake, alikuwa akitaniwa na watu wa kijiji chake wakimuita nyani ama sokwe, lakini baada ya hadithi yake kuchapishwa Februari, aligonga vichwa vya habari na kuwavutia wasamaria wema wengi , maisha yake game change.
Maisha ya Elie sasa yamebadilika baada ya kupokea misaada kutoka kwa wasamaria wema, kwa kujengewa nyumba mpya na kuishi sehemu nzuri.
Kwa sasa anatajwa kama mtu maarufu /staa ,na huvalia suti za gharama kwelikweli huku akiwa na mashabiki wengi, yaani kila anapoonekana tu barabarani, kila mtu anataka kupiga picha naye.
Katika moja ya mahojiano, mama yake Elie alisema mvulana huyo alikuwa jibu la maombi yake baada ya kukata tamaa kuwa hawezi tena kupata watoto baada ya kupoteza watoto wake wa 5, na mtoto wake huyu hakuwa na uwezo wa kuzungumza na alikuwa na ugumu wa kusoma.
Elie Alipelekwa shuleni kufunzwa jinsi ya kuishi na watu baada ya miaka mingi ya kuishi msituni. Ama kwa Hakika “Mungu si Mzee Mkumba…”