POLISI ya Kiislamu katika Jimbo la Kano inayofahamika kama Hisbah imemkamata mwanaume mwenye umri wa miaka 26 kwa jina Aliyu Na Idris ambaye taarifa yake imekuwa ikienea kwenye mitandao ya habari ya kijami wikendi iliyopita kwa kutangaza kuwa anataka anunuliwe akidai kuwa amechoka na umasikini.
Kamanda wa Hisbah Harun Ibn Sina amesema kuwa kitendo alichofanya Aliyu ni kinyume ha sheria. ‘’Tumemkata na tunaendelea kumshikilia, kile alichokifanya kinazuiwa katika Uislamu, huwezi kujaribu kujiuza hata uwe katika hali gani.”
Aliyu ambaye ni fundi nguo amekuwa akizungumza na waandishi wa habari nchini Nigeria, akisema kwamba alikuwa na matatizo makubwa ya kifedha, ndio maana akaamua kujiuza kwa naira milioni 20 (Tsh 112.46) ambayo ni bei aliyokuwa ameichapisha kwenye bango alilotembea nalo kwa mtu yeyote ambaye angempatia maisha yake yote.
“Nitawapa wazazi wangu Naira milioni 10 (Tsh 56.23). Pia nitalipa naira milioni tano (Tsh 28.12) kama kodi ya jimbo kama wataninunua ($12,000; £9,000), nitampatia naira milioni 2 ($5,000; £4,000) mtu aliyenisaidia kutangaza kuuzwa kwangu. Na pesa zitakazobaki nitazitumia kufanya biashara kwa ajili ya kujikimu katika maisha yangu ya kila siku,” amesema Aliyu.
Social Plugin