Profesa. Benard Chove akitoa salamu za Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kwa niaba ya Makamu Mkuu wa chou hicho Profesa. Raphael Chibunda.
Waziri wa Kilimo,Umwagiliaji na mifugo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Soud Hassan (katikati) akimkabidhi cheti cha pongezi kwa kufanisha mkutano huo mkubwa Profesa. Benard Chove kwa niaba ya SUA.
Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia hotuba za ufungaji wa mkutano huo wa pili wa kitaifa wa Kilimo Hai.
Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia hotuba za ufungaji wa mkutano huo wa pili wa kitaifa wa Kilimo Hai.
Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia hotuba za ufungaji wa mkutano huo wa pili wa kitaifa wa Kilimo Hai.
Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia hotuba za ufungaji wa mkutano huo wa pili wa kitaifa wa Kilimo Hai.
Mkutano ukiendelea.
Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia hotuba za ufungaji wa mkutano huo wa pili wa kitaifa wa Kilimo Hai.
Na Calvin Gwabara, Dodoma
IMEBAINISHWA kuwa wakulima wengi nchini hawana uwezo wa kumudu gharama za kununua madawa na mbolea kwa ajili ya kustawisha mashamba na kuua wadudu na magonjwa kwenye mazao yao hivyo kilimo Ikolojia kinaweza kuwa msaada mkubwa kwao.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Kilimo,Umwagiliaji na mifugo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Soud Hassan kwa niaba ya Waziri wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda wakati akifunga Kongamano la Pili la kitaifa la Kilimo Hai lililofanyika kwa siku mbili Jijini Dodoma na kuwakutanisha wadau wote wa Kilimo Hai kutoka nani nan je ya Tanzania.
“Niwatake wadau wote wa kilimo Hai nchini kuhakikisha malighafi zinazozalishwa za kuulia wadudu na magonjwa pamoja na mbolea ziweze kupatikana kwa wingi, kwa urahisi na kwa bei nzuri kwenye maeneo mbalimbali nchini ili ziweze kuwafanya wakulima wetu waachane na matumizi makubwa ya madawa na mbolea za viwandani” alisema.
Amewahakikishia kuwa Serikali ya Tanzania iko pamoja na wadau wote wa kilimo Hai na imeiweka katika mipango yake na ili kuendana na mabadiliko ya tabia nchi mbegu stahimilivukwa uhakikika wa chakula lishe na kuongeza kipato zinahitajika.
Waziri huyo wa Kilimo Zanzibar alisema serikali sikivu ya Tanzania imetengeneza mazingira rafiki ya Kilimo Hai kupitia sera yake ya kilimo ya mwaka 2013 na inatambua mchango wa utafiti wa kilimo Hai kupitia wanafunzi wa Shahada za Uzamili na uzamivu wa Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA.
“Malengo makubwa ya Wizara ya kilimo ni Utafiti,Tija ya uzalishaji,Upatikanaji wa Pembejeo husasani mbolea viutilifu,mbegu bora na zana za kilimo,Masoko ya mazao,Uongezaji thamani wa mazao na Miundombinu ya umwagiliaji”alisisitiza Hassan.
Aidha amesema Tanzania ina wakulima wa Kilimo Hai waliosajiliwa wanafikia wakulima 600,000 na kwa idadi hiyo kubwa ni vyema TOAM kuendelea kuwatambua na kuwasjili ili kuendelea kuwatumia kwa lengo la kuzalisha chakula.
Akitoa salamu za Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Benard Chove kwa niaba ya Makamu Mkuu wa chou hicho Jukumu la SUA Prof. Raphael Chibunda amesema jukumu la SUA ni kuchangia katika maendeleo ya nchi kwa kufanya mafunzo, utafiti na kutoa huduma kwa jamii.
”Ni matumaini yangu washiriki kutoka SUA wameweza kutoa maelezo kuhusu shughuli mbalimbali zilizofanyika na zinazoendea kufanyika katika kuhakikisha Chou kinatoa mchango wake katika kuendeleza Kilimo ikolojia kupitia mafunzo utafiti na ushauri, alibainisha Profesa Chove.
Prof. Chove amesema kuwa chuo kimeendelea kuyaishi maono na malengo na maagizo ya Baba wa Taifa ya kuanzisha chuo hicho na kusema kuwa maza yao ni Wanafunzi wanzalishwa chuoni hapo na humu ndani nikisema wote waliopita SUA wasimame naamini itakuwa vurugu kubwa sidhani kama kuna watakaobaki kwenye kiti hivyo tumeendelea kuishi kwenye maono yake.
Ameedelea kusema kuwa yote ambayo SUA imeyatekeleza kwa kipindi chote hicho toka kuanzishwa kwake juu ya mafunzo na kuchangia katika maendeleo ya Kilimo Ikolojia yasingeweza kufanyika bila ushirikiano ambao wameupata kutoka kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wadau mbalimbali wa maendeeo.
“Hivo napenda kuwashukuru wadau wetu wa maendeleo kama vile Serikali ya Denmark kupitia mradi wa BSU,SWISSAID,Wakfu wa MACKNIGHT kutoka Marekani,Shirika la Maendeleo la Ubelgiji na Asasi zingine zisizo za Kiserikali na wengine wengi.
“Napenda kuchukua nafasi hii kuwahakikishia kwamba chuo kitaendelea kutoa ushirikiano na kufanya kila linalowezekana kuhakikisha malengo ya ushirikiano wetu yanafanikiwa kwa manufaa ya watanzania wote na Taifa”. alisema.
Profesa Chove amesema miongoni mwa mafanikio ya ushirikiano na wadau hao ni kaunzisha Shahada ya Uzamivu Kilimo Ikolojia ambayo imeingia mwaka wa pili lakini mandalizi ya kuanzisha Shahada ya umahili ya Kilimo Ikolojia yanaendelea na hii itasaidia kuboresha na kujenga uwezo zaidi kwa chuo katika kutoa huduma kwa jamii.