LATRA CCC YADHAMIRIA KUONDOA KERO ZA WATUMIAJI WA USAFIRI ARDHINI


Naibu waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi,Mhe.Mwita Waitara akifurahi mara baada ya kuzindua Tovuti ya Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe.Mwita Waitara akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Tovuti ya Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) leo Jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe.Ng`wilabuzu Ndatwa Ludigija akifuatilia hafla ya uzinduzi wa Tovuti ya Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) leo Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Bodi ya LATRAA CCC, Dkt.George Makuke akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Tovuti ya Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) leo Jijini Dar es Salaam.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la LATRA CCC, Bw.Leo Ngowi akifuatilia hafla ya uzinduzi wa Tovuti ya Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) leo Jijini Dar es Salaam

Baadhi ya wadau wa LATRA CCC wakifuatilia Uzinduzi wa Tovuti ya Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) leo Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wadau wa LATRA CCC wakifuatilia Uzinduzi wa Tovuti ya Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) leo Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wadau wa LATRA CCC wakifuatilia Uzinduzi wa Tovuti ya Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) leo Jijini Dar es Salaam. Naibu waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe.Ng`wilabuzu Ndatwa Ludigija (waliokaa katikati), Mwenyekiti wa Bodi ya LATRAA CCC, Dkt.George Makuke (wa kwanza Kushoto), Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la LATRA CCC, Bw.Leo Ngowi (wa kwanza kulia) wakipata picha ya pamoja na watumishi wa LATRAA CCC wakati wa Uzinduzi wa Tovuti ya Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) leo Jijini Dar es Salaam. Naibu waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe.Ng`wilabuzu Ndatwa Ludigija (waliokaa katikati), Mwenyekiti wa Bodi ya LATRAA CCC, Dkt.George Makuke (wa kwanza Kushoto), Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la LATRA CCC, Bw.Leo Ngowi (wa kwanza kulia) wakipata picha ya pamoja na askari wa usalama barabarani wakati wa Uzinduzi wa Tovuti ya Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) leo Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

********************************

NA MWANDISHI WETU

Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) limedhamiria kuondoa kero za wasafiri wa Ardhini kwa kutoa elimu katika maeneo mbalimbali itakayosaidia kuondokana na kero ambazo si za lazima.

Ameyasema hayo leo Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe.Mwita Waitara wakati akizindua Tovuti ya Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) ambayo ni www.latraccc.go.tz,

Amesema kuwa Baraza hilo teyari limeshaanza kutoa elimu ya kuwa wastaarabu wanapotumia vyombo vya moto kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwani visa vya wananchi kutumia madirisha kuingia kwenye vyombo vya usafiri zimepungua.

Hata hivyo Baraza hilo limesema kuwa Wananchi wameanza kuelekezwa kupanda mstari wanapoingia kwenye usafiri ili kupunguza baadhi ya kero zinazozuilika bila gharama yeyote.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la LATRACCC,Bw.Leo Ngowi amesema kuwa baraza la LATRA CCC linampango wa kuahamisha jamii kuingia kwenye vyombo vya usafiri kwa atakayekuwa wakwanza kufikia kituoni ndiye atakayekuwa wakwanza kupata huduma ya usafiri kistaarabu.

Hata hivyo amesema kuwa watoto, wajawazito, wazee na wagonjwa watapata huduma stahiki na kwa wakati.

Licha ya hayo Bw.Ngowi amesema kuwa wanataka kujenga jamii ambayo itakuwa na ustaarabu katika kutumia huduma ya usafiri hapa nchini pamoja na kuponya majeraha ya muda mrefu kwa abiria kwa kukaa muda mrefu vituoni.

Hivyo baraza la LATRA CCC limedhamiria kuepusha ajali na majeraha ya mwili kwa watumiaji wa usafiri wa aridhini pamoja na kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya kuambukiza.

Ngowi amesema kuwa licha ya kutoa elimu katika jamii kuwa ya kistaarabu lazima jamii iongeze utu, Umoja, upendo na Mshikamano ili kila mmoja aweze kutumia usafiri wa ardhini bila kuwa na kinyongo.

Amesema kuwa baraza la LATRA CCC wanaihimiza jamii kuanza kutumia kieletroniki katika sekta ya usafirishaji kama kutumia E-tiket kwa mabasi ya mijini na masafa marefu ili kuondoa kadhia ya wapiga debe.

Amesema watakusanya maoni kwa jamii juu ya mikinzano inayojitokeza katika sekta ya usafirishaji hapa nchini hasa kwa upande unaomwathiri mtumia huduma ya usafirishaji.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post