MAFUNZO YA SHERIA YA UDHIBITI UZITO WA MAGARI YA AFRIKA MASHARIKI YA MWAKA 2016 NA KANUNI ZAKE ZA MWAKA 2018 YAFUNGWA JIJINI DODOMA


Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Usalama na Mazingira, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Ujenzi), Mhandisi Kashinde Mussa akifunga semina ya mafunzo kwa wadau wa usafirishaji (hawapo pichani), kuhusu Sheria ya Udhibiti Uzito wa Magari ya Afrika Mashariki ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018 iliyofanyika katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.


Hakimu Mkazi Mfawizi mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Sylvia Lushashi akiteta jambo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Onesmo Lyanga pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Usalama na Mazingira, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Ujenzi), Mhandisi Kashinde Mussa, baada ya kuahirishwa kwa semina ya mafunzo ya Sheria ya Udhibiti Uzito wa Magari ya Afrika Mashariki ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018 kwa wadau wa usafirishaji, jijini Dodoma.


Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya Sheria ya Udhibiti Uzito wa Magari ya Afrika Mashariki ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018 wakimsikiliza mgeni rasmi, Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Usalama na Mazingira, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Ujenzi), Mhandisi Kashinde Mussa (hayupo pichani), wakati akifunga mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku moja katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.


Msimamizi wa Mizani kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Leonard Saukwa, akitoa elimu kwa wadau wa sekta ya usafirishaji, juu ya sheria ya Afrika Mashariki ya udhibiti wa uzito wa magari ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018, yaliyofanyika kwa siku moja katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.

Picha na WUU

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post