Mamia ya watu wamejitolea kuvua nguo zao na kubaki uchi ili kupigwa picha zinazoelezea namna Bahari ya Kifo (Dead Sea) inavyoendelea kukauka.
Katika halaiki hiyo ya wanawake kwa wanaume wapatao 300 nchini Israel, walionyeshwa wakiwa wamevaa nguo za ndani nyeupe na kuacha nje sehemu nyingine za miili zao. Hii ilikuwa kumpa nafasi mpiga picha Spencer Tunick, kuwapiga picha kama njia ya kuhamasisha watu kutunza bahari, BBC imeripoti.
Tunick, raia wa Marekani, amekuwa akiendesha kampeni hiyo katika maeneo tofauti ya fukwe za bahari duniani, kama vile eneo la barafu la Uswizi na ufukwe wa Afrika Kusini.
“Matembezi yangu nchini Israeli yamenipa uzoefu wa kipekee na ninafurahi wakati wote kurejea hapa na kupiga picha katika nchi pekee ya Mashariki ya Kati inayoruhusu sanaa ya aina hii,” alisema Tunick.
Upigaji picha huo ulihamasishwa na Wizara ya utalii ya Israeli.