Meneja wa Huduma kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bi. Honester Ndunguru akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma Mhe. Kanali Laban Thomas wakati timu ya maofisa kutoka TRA walipowasili wilayani humo kwa ajili ya kufanya kampeni ya elimu kwa mlipakodi.
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma Mhe. Kanali Laban Thomas akizungumza na maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) walipofika wilayani humo kwa ajili ya kufanya kampeni ya elimu kwa mlipakodi inayoendelea mkoani humo.
Afisa Msimamizi Mkuu wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. James Ntalika akimuelimisha mfanyabiashara wa Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma wakati wa kampeni ya elimu kwa mlipakodi inayoendelea mkoani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma Mhe. Kanali Laban Thomas (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) walipofika wilayani humo kwa ajili ya kufanya kampeni ya elimu kwa mlipakodi inayoendelea mkoani humo.
Afisa Msimamizi wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Shaga Gagunda akimuelimisha mfanyabiashara wa Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma wakati wa kampeni ya elimu kwa mlipakodi inayoendelea mkoani humo. (PICHA ZOTE NA TRA).
Social Plugin