Mkurugenzi mtendaji wa benki ya CRDB Tanzania,Abdumajid Nsekela,amewaomba viongozi wa dini kuzidisha upendo ,amani na utulivu kama Mtume Muhammad ( S.A.W.) alivyohamisha enzi za uhai wake.
Nsekela, alisema hayo leo wakati wa Maulid ya mazazi ya mtume Muhammad ( S.A.W) yaliyofanyika kitaifa Mkoani Kagera katika viwanja vya Kaitaba mjini Bukoba.
Alisema Mtume Muhammad ( S.A.W ) amesema katika Quran sura ya 4 Aya ya 59 watii wale wenye mamlaka kati yenu.
Alisema benki hiyo itaendelea kushirikiana na viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali katika kuijenga nchi kiuchumi.
Naye karibu mkuu wa Baraza la waislamu Tanzania ( BAKWATA ) Nuru Mruma , alisema waumini waendelee kuwaheshimu viongozi wa dini na wa serikali wenye mamlaka ya juu.
Kwa upande wake Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,alisema uislamu unahimiza amani ambayo ndiyo kila kitu katika maisha ya shule na kufanya maendeleo ili kila mmoja aweze kuishi na kufanya ibada salama.
Majaliwa, alisema Tanzania imekuwa nchi ya amani kwa miongo mingi na serikali inatambua madhehebu ya dini katika kuhamasisha amani na maendeleo.
Alisema pia taasisi za dini kutoa elimu na afya katika jamii zimekuwa mchango mkubwa katika serikali.
Alisema Serikali itaendelea kuunga mkono taasisi za dini na kudai kuwa viongozi wa dini wamekuwa mstari wa mbele kukemea maovu.
Social Plugin