Na George Mhina - Kahama
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeendesha mafunzo ya siku moja kwa Watendaji na Maafisa wa Serikali Wilayani Kahama mkoani Shinyanga kwa lengo la kuwajengea uwezo kuhusu kazi,wajibu na mafanikio ya EWURA katika udhibiti wa huduma za Nishati na Maji.
Mafunzo hayo ya siku moja yalifanyika leo tarehe 29 Mwezi wa Kumi ,2021 katika Ukumbi wa Manispaa ya Kahama na yalivudhuriwa wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Manispaa (CMT), TANESCO, RUWASA, Ofisa Madini na wanahabari.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kahama Bwana Timothy Ndanya akifungua mafunzo hayo, alisema watendaji wa serikali za Mitaa na Watendaji wengine kwenye ngazi za Wilaya ni wadau wakubwa wa EWURA katika utendaji wao wa kazi na kwamba EWURA kama taasisi ya Umma hatuna budi kushirikiana nayo ili kuweka kutekeleza majukumu Yao ya udhibiti kwa ufanisi.
Ndanya amesema elimu hii itayotolewa leo itusaidie watendaji katika kuwasaidia wawekezaji wanaotaka kuwekeza kwenye Manispaa ya Kahama na kutatua kero za wananchi kwenye sekta za nishati na maji.
Akitoa mada kwenye semina hiyo Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa Bw George Mhina amesema EWURA itaendelea kutoa ushauri kwa serikali katika kuandaa sera,sheria na kanuni zitakazowezesha kukua kwa sekta
za Nishati na Maji Nchini.
Aidha alisema ‘EWURA imesaidia kuzuia mfumko wa bei, kuimarisha mamlaka za maji nchini na kukuza umeme binafsi na kwamba itaendelea kuzingatia misingi mikuu sita ya utawala bora katika maamuzi ya udhibiti ambayo ni weledi, uwajibikaji, utabirikaji, ushirikishaji, uwazi na kufuata sheria’.
Bw Mhina amezitaka taasisi na makampuni yanayotoa huduma za nishati na maji katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kutoa huduma kwa wateja wao kwa ku zingatia sheria, Kanuni, mikataba ya huduma kwa Mteja na ma sharti ya leseni zao.
Kwa pande wake, Afisa Mkuu wa Uhusiano na Mawasiliano wa EWURA bwana Wilfred Mwakalosi alisema kuwa EWURA sikuzote imekuwa ikifanya kazi kwa ushiriano wa karibu na wadau wake ambao ni pamoja na Serikali za Mitaa.
Social Plugin