Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NIC YAZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA


Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Dkt. Elirehema Doriye akimlisha Keki Mkurugenzi wa Masoko na huduma kwa wateja kutoka Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw.Yessaya Mwakifulefule katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja katika ofisi za makao Makuu ya Shirika la bima la Taifa (NIC) leo Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Dkt. Elirehema Doriye akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja katika ofisi za makao Makuu ya Shirika la bima la Taifa (NIC) leo Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Dkt. Elirehema Doriye akizungumza na wateja walioweza kufika katika Shirika hilo, katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja katika ofisi za makao Makuu ya Shirika la bima la Taifa (NIC) leo Jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Dkt. Elirehema Doriye akikata keki katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja katika ofisi za makao Makuu ya Shirika la bima la Taifa (NIC) leo Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Dkt. Elirehema Doriye akikata keki katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja katika ofisi za makao Makuu ya Shirika la bima la Taifa (NIC) leo Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Dkt. Elirehema Doriye akimlisha keki mmoja wa wateja wa Shirika hilo, katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja katika ofisi za makao Makuu ya Shirika la bima la Taifa (NIC) leo Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Dkt. Elirehema Doriye akilishwa keki na mmoja wa wateja wa Shirika hilo, katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja katika ofisi za makao Makuu ya Shirika la bima la Taifa (NIC) leo Jijini Dar es Salaam. Mteja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw.Vedasto Rwegoshora akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja katika ofisi za makao Makuu ya Shirika la bima la Taifa (NIC) leo Jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa Masoko na huduma kwa wateja kutoka Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw.Yessaya Mwakifulefule akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja katika ofisi za makao Makuu ya Shirika la bima la Taifa (NIC) leo Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Dkt. Elirehema Doriye akimlisha Keki Mkurugenzi wa Masoko na huduma kwa wateja kutoka Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw.Yessaya Mwakifulefule katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja katika ofisi za makao Makuu ya Shirika la bima la Taifa (NIC) leo Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Dkt. Elirehema Doriye akiwahudumia wateja wa Shirika hilo waliofika kwaajjili ya kupatiwa huduma katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja katika ofisi za makao Makuu ya Shirika la bima la Taifa (NIC) leo Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Dkt. Elirehema Doriye akimlisha keki Mkurugenzi-Bima za Mali na Ajali (NIC) Bw.Ntimba Bunny katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja katika ofisi za makao Makuu ya Shirika la bima la Taifa (NIC) leo Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi-Bima za Mali na Ajali (NIC) Bw.Ntimba Bunny akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja katika ofisi za makao Makuu ya Shirika la bima la Taifa (NIC) leo Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*************************

NA EMMANUEL MBATILO,DAR ES SALAAM


Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Dkt. Elirehema Doriye amesema wataendelea kujitahidi kufanya maboresho zaidi ya huduma hasa kwa kuwajali wateja wao ambao ndio wadau wakubwa wa Shirika hilo.

Ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja ambayo hufanyika mwezi Oktoba kila Mwaka.Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ofisi za makao Makuu ya NIC Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kuzindua wiki ya huduma kwa wateja, Dkt. Doriye amesema kuwa uwepo wa shirika la Bima la Taifa linategemea sana wateja kwa maana ya wadau mbalimbali wanaopata huduma kutoka shirika hilo.

"Sisi tunawahaidi kufanya maboresho zaidi ya huduma, mojawapo ya kauli mbiu yetu inayosema Mteja kwanza tutaweka katika kila shughuli zetu wateja na sehemu ya kwanza kabisa." Amesema Dkt. Doriye

Amesema wiki hii kwa pamoja na wateja washeherekee, wafurahie lakini kuwa alama ya kuonesha Shirika hilo linasimama kwaajili ya wateja wao, na kutoa elimu juu ya umhimu wa bima.

"Ni muhimu jamii na wateja wote wa bima kujua kuwa sisi ndio bima." amesisitiza Dkt. Doriye.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Masoko na huduma kwa wateja kutoka Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw.Yessaya Mwakifulefule amesema kuwa wanatambua mchango wa wateja wao hivyo kuna umuhimu wa kuboresha huduma zao.

"NIC tunaamini na kutambua kuwa wateja wetu ni zaidi ya wateja, Wao ndio chanzo cha biashara na mafanikio ya nchini hii hivyo tupo kwaajili ya kuwahudumia wateja wetu." Amesema Mwakifulefule.

Pamoja na hayo Bw.Mwakifulefule amewasisitizia wadau wa Shirika hilo kuendelea kutumia huduma zinazotolewa na NIC kwa maendeleo ya Taifa na ndo maana wanasema "NIC ni Bima la Taifa".

Nae mmoja wa wateja wa NIC, Bw.Vedasto Rwegoshora ameipongeza NIC kwa kutambua umuhimu wa wateja wake na kuhakikisha linawajali wateja hivyo amewaomba kuendelea kuhakiksha wanatoa huduma bora ambazo zitawafanya wateja kujivunia na huduma zinazotolewa na NIC.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com