NMB TANGA YAFUNGUA FURSA KWA WANAMICHEZO

 

MENEJA wa NMB  Tawi la Madaraka Jijini Tanga ambaye pia Mwenyekiti wa Mameneja wa Benki hiyo mkoa wa Tanga ,Elizaberth Chawinga akizungumza na waandishi wa habari
MENEJA wa NMB  Tawi la Madaraka Jijini Tanga ambaye pia Mwenyekiti wa Mameneja wa Benki hiyo mkoa wa Tanga ,Elizaberth Chawinga akizungumza na waandishi wa habari Jijini Tanga .


NA OSCAR ASSENGA,TANGA.

BENKI ya NMB imefungua milango kwa wanamichezo mkoani Tanga ambao wanashiriki kwenye michezo mbalimbali iwapo wanataka sapoti kutoka kwao waende wakawaone ili kuweza kuona namna gani wanaweza kuwasaidia vijana kuweza kuinua na kukuza vipaji vyao.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Mameneja wa Mkoa wa Tanga NMB Elizaberth Chawinga wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa Mashindano ya Ligi ya Kikapu ya NMB Madaraka Cup iliyoshirikisha timu kutoka mkoa mzima wa Tanga.

Chawinga ambaye pia ni Benki ya NMB tawi la Madaraka Jijini Tanga alisema wao waende wakawaone Mameneja hao wakiona kama hawapati sapoti  wawasiliane naye aone namna ya kuzungumza na wenzake na kwenye vikao vyao wataelezana ni vizuri kuwasaidia vijana.

“Ni vizuri tuwasaidia vijana kwa sababu wao Benki ya NMB wapo karibu na wananchi kama ilivyo kauli mbiu yao ya NMB karibu yao hivyo ni vema kuweza kutoa mchango wao kuwasaidia kuweza kutumiza ndoto zao za mafanikio kupitia michezo”Alisema

“Lakini tunafurahi kuhimitisha mashindano ya Kikapu ya Madaraka NMB Basket Ball Cup yaliyoshirikisha timu za mkoa wa Tanga yalikuwa yanafanyika Jumamosi na Jumapili timu nyingi zilishiriki sisi kama NMB tuna furaha kufanikisha hilo kwa sababu tulikuwa wadhamini wakuu”Alisema

Aliongeza lakini pia wametoa zawadi kwa washindi na wamelisimamia vizuri na wanapenda kuwatia moyo vijana wengine wa mkoa wa Tanga kuweza kuandaa mashindano na wao wakadhamini kutokana na kwamba furaha yao ni kurudisha kwenye jamii ya Tanga hivyo kama vijana wengine wachangamkie fursa ya kushiriki kwenye michezo mengine.

“Hivyo nitoe wito kwa vijana wa kike nao waweze kuandaa Ligi ya Basketball kwa wanawake  na sisi tunaweza kuwashika mkono ..lakini niseme mwamko wa michezo kwa mkoa wa Tanga ni mkubwa na serikali iliangalie kwa sababu vijana wanakosa ufadhili”Alisema

Meneja huyo alisema ukiangalia hata nyakati za jioni kuna vijana wengi wanashiriki mazoezi kwenye viwanja mbalimbali na  hata wenye vituo vya kukuza soka wanaweza kuja kuangalia huku Tanga kwani vijana wapo vizuri sana kwenye michezo.

Hata hivyo alisema vijana hao wapo vizuri kwenye soka na wana mwamko ni mkubwa hivyo  kama kuna wadau wanaweza kuona namna ya kusaidia vipaji vikaleta mafanikio makubwa kwenye timu zetu za Taifa za Tanzania katika siku za baadae.

“Kwani mkoa wa Tanga ni mikoa yenye sifa ya kutoa wachezaji mahiri wa soka hapa nchini kama John Bocco wa timu ya Simba,Bakari Mwamnyeto anayechezea timu ya Tanga na Abdul Selemani Sopu yupo aliyepo kwenye kikosi cha kwanza cha timu ya Taifa hivyo Tanga tupo vizuri lakini wanakosa sapoti na tunamuomba Mbunge wetu Ummy Mwalimu aliangalie kwa jicho la pili”Alisema

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post