Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA : SERIKALI INAKAMILISHA VIGEZO VINAVYORUHUSU CHATO KUWA MKOA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akilihutubia Taifa kwenye kilele cha mbio za Mwenge Maalum wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021 zilizofanyika leo Oktoba 14,2021 katika Uwanja wa Magufuli Wilayani Chato Mkoani Geita.
Kiongozi wa mbio za Mwenge Maalum wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021 Luteni Josephine Paul Mwambashi akikabidhi Mwenge Maalum wa Uhuru kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe. Samia Suluhu Hassan, baada ya kufikia kilele cha mbio za Mwenge huo Maalum kwa Mwaka 2021 leo Oktoba 14,2021 katika Uwanja wa Magufuli Wilayani Chato Mkoani Geita.

****
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema serikali inakamilisha vigezo vinavyoruhusu Chato kuwa Mkoa.

Rais Samia ameyasema hayo kwenye kilele cha mbio za Mwenge Maalum wa Uhuru kwa Mwaka 2021 leo Oktoba 14,2021 katika Uwanja wa Magufuli Wilayani Chato Mkoani Geita.

"Chato bado haujawa mkoa, kuna vigezo kadhaa ambavyo bado tunaendelea kuviangalia...na vigezo hivi vikikamilika hili jambo linakamilika",amesema Rais Samia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com