Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema amewataka viongozi mbalimbali serikali kwenda kutumikia wananchi kuleta maendeleo huku akisisitiza kuwa hatarajii kuona mkuu wa mkoa anakuwa mla rushwa na kugeuka Miungu watu.
Rais Samia ameyasema hayo leo Jumatatu Oktoba 11,2021 wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema.
"Uongozi ni dhamana siyo zawadi, na kama ni dhamana ina miiko yake, sheria na kanuni zake. Tunategemea viongozi mtakuwa mfano, sitegemei kuona mkuu wa mkoa anaingia kwenye vitendo vya rushwa, sitegemei kuona wakuu wa mikoa mnakuwa Miungu watu huko mliko. Kazi zenu zina miiko, miongozo na sheria ambazo mnatakiwa mzirejee na kuzifuata...mpo kule kutumikia watu, siyo watu wawatumikie nyie. Naomba mkafanye kazi zilizowapeleka huko",amesema Rais Samia.
"Samia Suluhu Mimi ninakotoka hakuna Makabila, kwetu kule Zanzibar tunajuana kwa maeneo lakini hata kwenye system ya makuzi, Shule na Siasa tunamshukuru sana sana Baba wa taifa letu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ametukuza bila kuangalia Makabila yetu",amesema Rais Samia.
"Na Mimi hapa siangalii Kabila kwenye utendaji kazi wangu. Sasa watu wanafanya makosa ukiwashika, ukiwawajibisha umewajibisha kwa sababu ya kabila flani mimi sina kabila, na kwa maana hiyo hata kwenye utendaji wangu wa kazi. Ukikosea kwenye kazi mimi na wewe wala sitakufumbia jicho..sasa kama umetoka huko ulikotoka ukijivunia wewe ni kabila flani,mimi sina kabila Mwalimu Nyerere alitufundisha kufanya kazi bila kuangalia makabila na ndicho ninachokifanya..
Kwa hiyo muende mkafanye kazi, mfanye kazi mkifanya majambo yasiyofaa, mkishikwa kwa sababu ya kabila flani.... ukilikoroga nakutumbua bila kuangalia kabila, anayekosea nitamuondoa, sipangi kwa kuangalia kabila, napanga kwa uwezo wake ili kwenda kusaidia wananchi kuleta maendeleo",amesema Rais Samia
Social Plugin