Mkurugenziwa Sera na MipangoWizarayaKilimo Bwana Obadiah Nyagiro akiwasilisha hotuba yake kwa wadau wa APRA
Mkuu
wa Mradi wa APRA na Mtafiti kutoka Chuo Kikuu Cha Sokoine cha Kilimo SUA Profesa Aida
Isinika akiwasilisha matokeo ya tafiti kwa wadau.
Mtafiti kutoka Chuo
Kikuu Cha Sokoine cha Kilimo SUA Profesa Mtengua Mdoeakichangia jambo kwenye kikao hicho.
Dk. Christopher Magomba Mhadhiri na Mtafiti katika mradi huo kutoka Chuo Kikuu Cha Sokoine
cha Kilimo SUA
akitoa maelekezo mafupi kuhusiana na tafiti.
Wadau wakifatilia wasilisho la matokeo ya Utafiti wa APRA.
Wadau wakifatilia wasilisho la matokeo ya Utafiti wa APRA.
Wadau wakifatilia wasilisho la matokeo ya Utafiti wa APRA.
Wadau wakifatilia wasilisho la matokeo ya Utafiti wa APRA.
Wadau wakifatilia wasilisho la matokeo ya Utafiti wa APRA.
Wadau wakifatilia wasilisho la matokeo ya Utafiti wa APRA.
Wadau wakifatilia wasilisho la matokeo ya Utafiti wa APRA.
Wadau wakifatilia wasilisho la matokeo ya Utafiti wa APRA.
Wasilisho likitolewa
Wasilisho likitolewa
Wadau wakifatilia wasilisho la matokeo ya Utafiti wa APRA.
Na Amina Hezron - Dodoma
SERIKALI kupitia Wizara ya Kilimo imekishukuru Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa jitihadakubwa ambazo watafiti wake wanazifanya katika kufanya tafiti mbalimbali zenye tija za kilimo zikiwa na lengo la kusaidia kuboresha kilimo, kuinua maisha ya watanzania na kuinua pato la taifa.
Akizungumza kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu waWizara ya Kilimo, Mkurugenzi wa Sera na MipangoWizara ya Kilimo, Obadiah Nyagiro katika Warsha ya Kitaifa ya kutoa mrejesho wamatokeo yautafiti Mradi wa Utafiti wa Sera za Kilimo BaraniAfrika (APRA) liyofanyika leo mkoani Dodoma amepongeza kazi kubwa iliyofanywa na watafitikwenye mradi huo na hasa kitendo chao cha kuamuakurudisha matokeo ya utafiti wao walengwa.
“Bila Utafiti hakuna jambo jipya lenye maamuzi yakiserikali linaweza kutokea, kama kuna matamkoyametoka bila utafiti utekelezaji wake hauwezi ukazaa mambo ambayo ni sahihi ambayo yanaweza yakaletamaendeleo kwa Wananchi, hivyo ni vizuri tafitizifanyike na mabadiliko ya sera yafanyike kulinganana uchambuzi uliofanyika” alisema Nyagiro.
Aidha Nyagiro ameeleza kuwa mipango yaSerikali hivi sasa inahimiza kilimo cha alizeti nchiniili kupunguza uhaba wa upatikanaji wa mafuta ya kulana kwa mwaka huu wa Serikali imedhamiria kusisitiza kuongeza Kilimo cha alizeti katika mikoa yaDodoma na Singida na inaongeza bajeti ya utafiti kwaTaasisi ya Utafiti wa Kilimo(TARI) na kuwezeshawakala wa mbegu nchini ( ASA) ili kusaidia mbegubora za alizeti zinapatikana kwa wingi.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo wa Sera naMipango Wizara ya Kilimo alisema zao la mpungani muhimu kwa usalama wa chakula hivyo Serikali inahimiza
sekta binafsi kushirikiana na serikali kuwekeza katika miundombinu ya umwagiliaji ili uzalishaji wa mpunga ufanyike angalau mara mbili kwa mwaka.
Akielezea matokeo ya tafiti hizo Mtafiti wa Utafiti huo kutoka (SUA) Prof John Jeckonia alisema kuwamatokeo makubwa ambayo tafiti imebaini kuwa kilimocha
alizeti kimeleta mchango mkubwa katikakupunguza umasikini kwa kuongeza vipato vya watu.
Alisema fursa mpya zimeibuka kutokana na kilimohicho na kwamba wapo waliopata manufaa kutokakatika kilimo hicho cha alizeti kuanzisha shughurinyingine za
kiuchumi ambazo pia zinamanufaamakubwa kwa maisha yao.
“ili kuondoa changamoto zilizopo kuna mambo kadhaayanatakiwa kufanyika, kwanza kuongeza huduma za ugani,upatikanaji wa pembejeo za kisasa,kuongeza
tijakwa maeneo,kuwahakikishia wakulima masokokwakuwa soko na bei ndo kitu kinachowavutiawakulima kuzalisha zaidi kwakuwa wakiwa na uhakika wa
kuuza kwa bei bora wanaweza wakavutiwa zaidikutumia mbegu za kisasa ambazo ni ghali kulinganishana mbegu za kienyeji lakini ambazo uzalishaji wake kwa
tija ni mkubwa na ni mzuri “ alifafanua Profesa Jeckonia.
Mtafiti na Mkuu wa Mradi wa APRA, Profesa Aida Isinika kutoka SUA ameiomba NEMC kufuatilia ili kuhakikisha mazingira yanakuwasalama katika Wilaya ya Kilombero kutokana na matumizi mabaya ya viuatilifu hasa viua maguguyanayofanywa na wakulima ambayo yasipodhibitiwayanaweza kuleta athari kwa afya zao na mazingira pia.
“Matumizi ya viau magugu yanawasaidia kupunguzakazi lakini matumizi yale yanatumika kwa njia ambayosi sahihi kwa hiyo inawezekana huko mbele
tukapata matatizo makubwa” alieleza Profesa Isinika.
Aliongeza”si hivyo tu, kupanuka kwa Mashaba yampunga kuna athari kwenye mabwawa yanayotumikakutengeneza umeme hivyo tunaweza tukapanua lakini tukawa na madhara ya kufanya uharibifu kule hivyohayo ni mambo yanayotakiwa kufanyiwa kazi”.
Utafiti umefanyika tangu mwaka 2017 naunategemewa kukamilika mapema mwakani na teyariumeshafanyika katika nchi sita ambazo ni Tanzania, Ethopia, Malawi, Zimbabwe, Ghana na Nigeria kwa kujikita kuchambua mmbo ya kisera yanayowezesha au kuhamasisha kilimo endelevu na shirikishi.
Hizo zote ni kujuhudi za kuboresha Maisha ya wadaukatika minyororo ya thamani ya kilimo ambapo kwahapa Tanzania utafiti huu uliratibiwa na watafiti kutokaChuo Kikuu Cha Sokoine cha Kilimo SUA katikawilaya ya Kilombero wakijikita katika zao la mpungana wilaya za ikalama na Iramba kwa zao la alizeti.
Social Plugin