Mtafiti Mbobezi kwenye Tafiti za Kilimo Hai kutoka SUA Prof. Kalunde Sibuga akiwasilisha maelezo yake kuhusu mchango wa SUA katika kutekeleza maazimio ya Mkutano wa kwanza wa Kitaifa wa Kilimo Hai wa mwaka 2019.
1.
Mratibu
wa Mradi Kitovu cha kilimo Ikolojia Tanzania Prof. Dismas Mwaseba kutoka Chuo
Kikuu cha Kilimo akitoa mrejesho wa mjadala wa mifumo wa chakula.
1.
Prof.
Anthony Zozimus kutoka Chou Kikuu cha Kilimo akichangia kwenye moja ya mijadala
katika Kongamano hilo la pili la Kilimo Hai.
1.
Mwanafunzi
wa Shahada ya Uzamili kutoka SUA anyefanya utafiti wa kuongeza uzalishaji wa
mpunga kwa kutumia mbinu mbalimbali za kiikolojia za kudhibiti magugu na
kuongeza rutuba kwenye udongo katika skimu ya Makwele Wilayani Kyela Mkoani
Mbeya akiwasilisha matoke ohayo mbele ya wadau.
1. Wadau wa kilimo Hai kutoka ndani na nje ya Tanzania wakifuatilia kongamano hilo.
1. Wadau
wa Kilimo Hai kutoka ndani na nje ya Tanzania wakifuatilia kongamano hilo.
Na Calvin
Gwabara - Dodoma
CHUO Kikuu
cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimeendelea kuwa kinara katika kufanya tafiti na uzalishaji wa wataalamu wa masuala ya kilimo
Hai hata kabla ya kuaizishwa kwa taasisi na mashirika
mbalimbali ambayo yanahamasisha na kusisitiza matumizi na faida za kilimo hai
nchini.
Hayo
yamesemwa na Mtafiti Mbobezi kwenye tafiti za Kilimo Hai kutoka SUA Prof.
Kalunde Sibuga wakati akiwasilisha maelezo yake kuhusu mchango wa SUA katika
kutekeleza maazimio ya Mkutano wa kwanza wa kitaifa wa Kilimo hai wa mwaka 2019
kwenye mkutano wa pili unaoendelea Jijini Dodoma.
“Katika
shahada ya kwanza tumekuwa na mtaala wa kilimo Hai Hata kabla ya Mkutano wa
mwaka 2019 na mataala ulilenga wanafunzi wanaochukua shahada ya kilimo pamoja
na ile ya Bustani na Mbongamboga, na huu mtaala bado upo kwahiyo tulianza
zamani” alifafanua Prof. Sibuga.
Alisema kila
mwaka Nchini Uganda kumekuwa kukiendshwa mafunzo ya muda mfupi ya kilimo Hai na
Chuo kwa kutambua umuhimu wake kimekuwa kikiwapatia wanafunzi wake ruhusa ya
kwenda kuhudhuria na kuonea ujuzi na kisha kurejea kuendelea na masomo na
mitihani yao.
Prof. Sibuga
amesema kuwa kupitia pia Mradi wa kujenga Vyuo imara (BSU) wamefanikiwa kuwezesha
kupatikana kwa mtaala kwa Wanafunzi wa Shahada ya Uzamivu mtaala ambao wadau
mbalimbali walishirikishwa katika kuuboresha na kuwezesha kuwapa nafasi ya
kusoma darasani lakini pia kuwepo kwa sehemu ya utafiti .
Sambamba na
hilo pia tayari wanao mtaala mwingine wa Shahada ya Uzamili ambao
umeshatengenezwa na sasa upo kwenye hatua mbalimbali za kuboreshwa na wadau ili
uweze pia kupitishwa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) kabla ya kuanza kutumika.
Pia Mtafiti
huyo amesema pamoja na mambo hayo lakini SUA na watafiti wake wamekuwa na
miradi kadhaa ya kilimo hai na kilimo ikolojia kama mradi wa uzalishaji na
ukuaji wa mnyororo wa thamani za mazao ya kilimo Hai ambao walikuwa
wanshurikiana na watafiti wengine wa afrika mashariki ambapo vijana wawili
walipata shahda za Uzamili na wengine wawili walipata shahada zao za uzamivu.
Prof. Sibuga
amesema kutokana na umuhimu huo hivi sasa SUA ina takribani miradi minne ya
kilimo Hai ambayo inatekelezwa kwenye maeneo mbalimbali nchini.
Mratibu wa Mradi Kitovu cha Kilimo Ikolojia Tanzania Prof. Dismas Mwaseba
kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo akitoa mrejesho wa mjadala wa mifumo wa chakula
amesema kuwa walifanikiwa kufanya mkutano ambao wadau mbalimbali walishiriki
katika kuongeza mapokeo ya kilimo Ikolojia na kilimo Hai nchini.
Prof.Mwaseba
amesema mambo mbalimbali yalijadiliwa lakini hasa ni katika Utafiti,Sera,
Uenezwaji wa matokeo na ushawishi ambapo amesema katika sera yalijadiliwa mambo
mengi lakini ilibainika kuwa Sera za kilimo nchini hazijazungumzia maswala ya
kilimo Ikolojia na kilimo Hai.
“Wadau
wamependekeza kwenye mkutano huo kuwa kwenye swala la utafiti na mafunzo iwepo
mitaala kwenye taasisi za elimu hasa vyuo vy akilimo ambayo itafundisha maswala
ya kilimo Ikolojia na Kilimo hai kwa mapana yake na kuwa kuna haja ya kufanya
utafiti kubainisha mahitaji ya wadau mbalimbali kwakuwa sasa tafiti zilizopo
zimegusa wadau maalumu tu hasa wa kilimo cha mboga” alieleza Prof. Mwaseba.
Mratibu huyo
wa Mradi wa Kitovu cha Kilimo Ikolojia amesema pia kuwa wadau wanapendekeza
kuwepo na ushawishi ambao utatokana na Ushahidi wa Kiutafiti na hasa zile
teknolojia mbazo zimethibitika kwa ubora wake na utangazaji wa bidhaa za Kilimo
ikolojia uzingatie mahitaji ya soko.
Ameongeza
kuwa uratibu wa kilimo ikolojia ufanisi uongezeke ili kusaidia wadau wa kilimo
ikolojia ili kuhakikisha wadau wa kilimo hicho wakuwa karibu katika kuendeleza lakini
pia wakushauri Kitovu cha kilimo ikolojia kipewe kazi ya kuratibu maswala hayo.
Prof.
Mwaseba alibainisha kuwa wadau wa mkutano huo walisema Kitovu cha kilimo
ikolojia kinaweza kufanikisha maswala mbalimbali ya sera,uwezeshaji pamoja na
utafiti ambapo katika kikao hicho wadau walipendekeza sasa kwakuwa mradi
unaisha basi kianzishwe kitovu cha kilimo Ikolojia na wadau wote waweze
kujiunga na kuchangia katika kushughulikia maswala mbalimbali ambayo yanakigusa
kilimo hicho nchini.
Katika Kongamano hilo la pili la kitaifa la kilimo Hai nchini Wanafunzi mbalimbali wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) wanaofanya Tafiti zao katika maswala ya Kilimo Ikolojia na Kilimo Hai wamepata nafasi ya kuwasilisha matokeo ya Tafiti zao na kujadiliwa na wadau hao lakini pia watafiti wa SUA nao wamewasilisha na kushiriki kwenye mijadala mbalimbali kuonesha ushiriki wao katika kuchangia ukuaji wa kilimo Hai nchini.