CHUO Kikuu cha Dodoma (Udom) kimemsimamisha kazi mhadhiri wa chuo hicho, Basil Mswahili kufanya majukumu yake yote ikiwa ni pamoja na kufundisha kwa tuhuma za rushwa ya ngono.
Tangu jana katika mitandao ya kijamii kumekuwa na ujumbe mfupi wa maneno ukionyesha kuwa mtumishi huyo kanaswa na mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho akitaka kupewa rushwa ya ngono ili amnasue katika mitihani ya marudio anayoifanya baada ya kufeli.
“Sio mmoja kuna wahadhiri kibao wanaofanya michezo michafu,” imeeleza sehemu ya ujumbe uliotumwa katika mtandao wa Twiter.
Katika taarifa iliyotolewa na kitengo cha mawasiliano kwa umma ya chuo hicho leo Alhamisi Oktoba 28, 2021 imesema kuwa Mswahili alisimamishwa tangu Oktoba 25 mwaka huu baada ya kupokea tuhuma hizo.
Amesema mhadhiri huyo amesimamishwa kufanya majukumu yote ikiwemo kufundisha hadi uchunguzi wa tuhuma hizo utakapokamilika. “Chuo kimekuwa kikichukua hatua stahiki za nidhamu kwa mujibu wa sheria na taratibu za kiutumishi bila kumwonea mtu,” amesema.
Social Plugin