Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Mhe.Bearice R. Dominic akipokea kiti cha mgonjwa kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof.William Anangisye mara baada ya kupokea leo msaada wa Viti hivyo vinne na mashuka 100 kwaajili ya wagonjwa katika Kituo cha Afya cha Kimara kilichopo Jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Mhe.Bearice R. Dominic akipokea mashuka kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof.William Anangisye mara baada ya kupokea leo msaada wa Viti vinne na mashuka 100 kwaajili ya wagonjwa katika Kituo cha Afya cha Kimara kilichopo Jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Mhe.Bearice R. Dominic akizungumza jambo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof.William Anangisye mara baada ya kupokea leo msaada wa Viti hivyo vinne na mashuka 100 kwaajili ya wagonjwa katika Kituo cha Afya cha Kimara kilichopo Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Mhe.Bearice R. Dominic akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya Hospitali katika Kituo cha Afya cha Kimara leo Jijini Dar ees Salaam.Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof.William Anangisye akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya hospitali katika Kituo cha Afya cha Kimara leo Jijini Dar es Salaam.Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha Dar es salaam-UTAFITI Prof.Benadeta Killian akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya hospitali katika Kituo cha Afya cha Kimara leo Jijini Dar es Salaam.Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ubungo Dkt.Peter Nsanya akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya hospitali katika Kituo cha Afya cha Kimara leo Jijini Dar es Salaam. Mganga Mfawidhi, Kituo cha Afya Kimara Dkt. Dickson Masele akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya hospitali katika Kituo cha Afya cha Kimara leo Jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Mhe.Bearice R. Dominic (katikati) akipata picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mganga mkuu wa Manispaa ya Ubungo na mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Kimara katika kukabidhi msaada wa vifaa vya hospitali kwenye Kituo cha Afya cha Kimara leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Mhe.Bearice R. Dominic (katikati) akiwa pamoja na baadhi ya Viongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mganga mkuu wa Manispaa ya Ubungo na mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Kimara wakipata picha ya pamoja na waandishi wa habari walioweza kuhudhulia kukabidhi msaada wa vifaa vya hospitali kwenye Kituo cha Afya cha Kimara leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Mhe.Bearice R. Dominic (katikati) akiwa pamoja na baadhi ya Viongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mganga mkuu wa Manispaa ya Ubungo na mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Kimara wakipata picha ya pamoja na wauguzi wa Kituo cha Afya cha Kimara katika hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya hospitali kwenye Kituo hicho leo Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
***********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Katika kuadhimisha miaka 60 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimetoa msaada wa shuka 100 viti vya kubebea wagonjwa 4 na vitakasa mikono katika Kituo cha Afya Kimara Dar es Salaam.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa hivyo Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof William Anangisye amesema maadhimisho hayo yatakuwa endelevu kwa mwaka wote wa masomo kwa kutoa vifaa mbalimbali kwa vituo vya Afya kuanzia Oktoba 25 mwaka huu.
"Chuo kinazidi kukua na idadi ya wanafunzi kuongezeka ambapo kwa sasa zaidi ya wanafunzi 43000 wanawake zaidi ya 19000 na kila mwaka tunapokea idadi kubwa ya maombi ya wanafunzi wanaotamani kujiunga zaidi ya mara mbili ya uhitaji wa chuo". Amesema
Hata hivyo amesema Chuo hicho kimeweka mikakati malengo, mipango na hatua tofauti kufikia ikiwemo ni pamoja na kuongezeka kwa duru ya za mahafali ya mwisho wa mwaka kuanzia mwaka 2021 kuboresha matokeo ya tafiti na ubunifu kutoka vyanzo vya ndani, ujenzi wa maabara na miundombinu ya kusomea.
Kitaendelea na maadhimisho haya kwa mwaka mzima kuanzia tar 25 oktoba 2021 kwa kutoa vifaa mbalimbali vya kiafya na kielimu kwa taasisi mbalimbali shule na hospital
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic ameshukuru chuo hicho kwa msaada huo kwani utawasaidia kwa kiasi kikubwa wahitaji na kujaza nafasi ambazo zilikuwa zinahitaji
Aidha amesema kwa siku kituo hicho kinahudumia watu wengi hivyo mahitaji ni makubwa kuliko eneo linavyoonekana na kutokana na ufinyu wa eneo ilibidi kijengwe kwa ramani tofauti na vituo vingine.
Hata hivyo amesema Halmashauri ya Ubungo bado inatoa fedha za mapato yake ya ndani kwa ajili ya upanuzi wake na wanasaidiwa pia na TANROAD na TAMISEMI na kikikamilika watahudumia watu wengi zaidi na kuboresha huduma ya Afya kwa jamii.