Meneja Masoko wa Kiwanda cha Maziwa cha Mama O Dairies, Josephat Vicent Massawe akionesha bidhaa 'Yoghurt na Mtindi' wanazozalisha katika kiwanda hicho kilichopo Bushushu Mjini Shinyanga.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wafanyakazi wa Kiwanda cha Maziwa cha Mama O Dairies kilichopo Bushushu Mjini Shinyanga wamepatiwa mafunzo kuhusu Teknolojia ya Maziwa ili kuongeza thamani ya mazao wanayozalisha ikiwemo Maziwa Halisi ya ng'ombe 'Mtindi', Yoghurt, Samli na Siagi.
Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa muda wa siku sita yamefungwa leo Ijumaa Oktoba 22,2021 katika kiwanda hicho yakiongozwa na Mwalimu Mstaafu wa Chuo cha SUA, Yahya Mrisho Watuta ambaye amebobea katika Teknolojia ya Maziwa.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo, Mtaalamu wa Teknolojia ya Maziwa, Yahya Mrisho Watuta amesema amefundisha kuhusu utengenezaji wa Yoghurt na Maziwa Halisi ya ng'ombe 'Mtindi' pamoja na mazao mapya kiwandani hapo ambayo ni Siagi na Samli.
“Nimetoa mafunzo kwa mazao mapya kama samli na siagi ambayo hayakuwepo katika kiwanda cha Mama O Dairies. Pia nimefundisha kuhusu muundo wa maziwa, na vinasaba vyake, ubora na usafi wa maziwa na teknolojia mpya mbalimbali kuhusu maziwa ikiwa ni pamoja na namna ya kupunguza gharama za uzalishaji”,amesema Watuta.
Watuta ambaye amekuwa akifundisha Teknolojia ya Maziwa kwa wajasiriamali wadogo nchini ameeleza kuwa Mazao mapya siagi na samli sasa yataingia Shinyanga, Kanda ya Ziwa na maeneo mengine nchini na kuingia kwenye soko la dunia kwani watu wengi wanapenda na wanahitaji bidhaa hizo.
“Mama O Dairies ambaye tayari ana Kiwanda cha Kusindika Maziwa aliniita kuja hapa Shinyanga kwa ajili ya kutoa mafunzo kuhusu teknolojia ya maziwa ili kusaidia kuboresha mazao yake. Kiwanda kilikuwa kinazalisha mazao lakini teknolojia waliyoipata sasa italeta mabadiliko makubwa zaidi na kuchochea uzalishaji na usambazaji wa mazao hayo”,ameeleza.
Kwa upande wake Mmiliki wa Kiwanda cha Mama O Dairies, Bi. Tabitha Amos Gityamwi ameshukuru kwa mafunzo yaliyotolewa na Mtaalamu wa Teknolojia ya Maziwa Bw. Yahya Mrisho Watuta ambayo yamewasaidia kujua vitu vingi zaidi kuhusu usindikaji maziwa hivyo kuongeza thamani zaidi katika mazao yao.
Naye Afisa Mifugo na Uvuvi wa Manispaa ya Shinyanga, Mohamed Mwalim Chamzhim amesema baada ya kutembelea kiwanda hicho alishauri apatikane mtaalamu wa Teknolojia ya Maziwa aliyebobea katika mazao ya maziwa awape mafunzo wafanyakazi wa kiwanda ili kuongeza thamani zaidi katika mazao wanayozalisha.
“Hiki kiwanda nimekuwa nikikilea naamini kitakuwa kikubwa zaidi ya hapa kilipo katika kiwango cha uzalishaji. Hivi sasa tupo katika taratibu za kuunganisha wafugaji walete maziwa ili kuongeza masoko ya mazao ya maziwa”,ameongeza.
Amewashauri wafugaji kuzalisha maziwa yenye ubora wakijua kwamba wanunuzi wao kwa taaluma waliyoipata wataweza kudhibiti ubora wa maziwa wakati wa kuyanunua hivyo kuwataka kuepuka kuchakachua maziwa.
Meneja Masoko wa Kiwanda cha Maziwa cha Mama O Dairies, Josephat Vicent Massawe amesema tayari bidhaa wanazozalisha ikiwemo Maziwa Halisi ya ng'ombe 'Mtindi' na Yoghurt zinapatikana katika Maduka na Super market mbalimbali huku akiwaomba wananchi kuboresha afya zao kwa kutumia bidhaa hizo ambazo zimetengenezwa kwa kuzingatia ubora unaotakiwa.
Amezitaja namba za mawasiliano kwa Kiwanda cha Maziwa cha Mama O Dairies kuwa ni 0759004004 au Email : mamaodairies@yahoo.com na unaweza kuwafuatilia kwenye mitandao ya jamii Facebook, Twitter na Instagram @mamaodairies na website ya www.mamaodairies.co.tz
Mtaalamu wa Teknolojia ya Maziwa, Yahya Mrisho Watuta akizungumza leo Ijumaa Oktoba 22,2021 wakati wa kufunga mafunzo kuhusu Teknolojia ya Maziwa ili kuongeza thamani ya mazao wanayozalisha ikiwemo Maziwa Mtindi, Yoghurt, Samli na Siagi. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Muonekano wa Maziwa Halisi ya Ng'ombe yanayozalishwa katika Kiwanda cha Maziwa cha Mama O Dairies, kiwanda hicho kilichopo Bushushu Mjini Shinyanga.
Muonekano wa bidhaa 'Yoghurt' zinazozalishwa katika Kiwanda cha Maziwa cha Mama O Dairies, kiwanda hicho kilichopo Bushushu Mjini Shinyanga.
Muonekano wa bidhaa 'Yoghurt' zinazozalishwa katika Kiwanda cha Maziwa cha Mama O Dairies, kiwanda hicho kilichopo Bushushu Mjini Shinyanga.
Mtaalamu wa Teknolojia ya Maziwa, Yahya Mrisho Watuta (katikati aliyeshikilia mazao mapya siagi na samli) akiwa na wafanyakazi wa Kiwanda cha Maziwa Mama O Dairies wakati wa kufunga mafunzo kuhusu Teknolojia ya Maziwa.
Afisa Mifugo na Uvuvi wa Manispaa ya Shinyanga, Mohamed Mwalim Chamzhim akizungumza leo Ijumaa Oktoba 22,2021 wakati wa kufunga mafunzo kuhusu Teknolojia ya Maziwa ili kuongeza thamani ya mazao wanayozalisha ikiwemo Maziwa Mtindi, Yoghurt, Samli na Siagi.
Mmiliki wa Kiwanda cha Mama O Dairies, Bi. Tabitha Amos Gityamwi akizungumza leo Ijumaa Oktoba 22,2021 wakati wa kufunga mafunzo kuhusu Teknolojia ya Maziwa ili kuongeza thamani ya mazao wanayozalisha ikiwemo Maziwa Mtindi, Yoghurt, Samli na Siagi.
Meneja Masoko wa Kiwanda cha Maziwa cha Mama O Dairies, Josephat Vicent Massawe akionesha bidhaa 'Yoghurt' wanazozalisha katika kiwanda hicho kilichopo Bushushu Mjini Shinyanga.
Meneja Masoko wa Kiwanda cha Maziwa cha Mama O Dairies, Josephat Vicent Massawe akionesha bidhaa 'Samli na siagi' wanazozalisha katika kiwanda hicho kilichopo Bushushu Mjini Shinyanga.
Afisa Mifugo na Uvuvi wa Manispaa ya Shinyanga, Mohamed Mwalim Chamzhim (katikati) akimkabidhi cheti cha kushiriki mafunzo ya Tekonolojia ya Maziwa Mmiliki wa Kiwanda cha Mama O Dairies, Bi. Tabitha Amos Gityamwi. Kushoto ni Mwezeshaji wa mafunzo hayo Mtaalamu wa Teknolojia ya Maziwa, Yahya Mrisho Watuta.
Afisa Mifugo na Uvuvi wa Manispaa ya Shinyanga, Mohamed Mwalim Chamzhim (katikati) akimkabidhi cheti cha kushiriki mafunzo ya Tekonolojia ya Maziwa mfanyakazi wa Kiwanda cha Mama O Dairies. Kushoto ni Mwezeshaji wa mafunzo hayo Mtaalamu wa Teknolojia ya Maziwa, Yahya Mrisho Watuta.
Afisa Mifugo na Uvuvi wa Manispaa ya Shinyanga, Mohamed Mwalim Chamzhim (katikati) akimkabidhi cheti cha kushiriki mafunzo ya Tekonolojia ya Maziwa mfanyakazi wa Kiwanda cha Mama O Dairies. Kushoto ni Mwezeshaji wa mafunzo hayo Mtaalamu wa Teknolojia ya Maziwa, Yahya Mrisho Watuta.
Afisa Mifugo na Uvuvi wa Manispaa ya Shinyanga, Mohamed Mwalim Chamzhim (katikati) na Mtaalamu wa Teknolojia ya Maziwa, Yahya Mrisho Watuta wakimkabidhi vitabu vya rejea kuhusu Teknolojia ya maziwa ,Meneja Masoko wa Kiwanda cha Maziwa cha Mama O Dairies, Josephat Vicent Massawe.
Afisa Mifugo na Uvuvi wa Manispaa ya Shinyanga, Mohamed Mwalim Chamzhim (kushoto) akizungumza baada kuonja utamu na radha ya Yoghurt inayozalishwa katika Kiwanda cha Mama O Dairies.
Cheers!