Picha ya bweni
Wanafunzi wanne wa Sekondari katika Kaunti ndogo ya Rabai, Kilifi nchini Kenya wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kuchoma moto bweni baada ya kuripotiwa kunyimwa ruhusu ya kutazama mchezo wa Manchester United dhidi ya Liverpool.
Kamanda wa Polisi, Fredrick Abuga amesema wanafunzi hao ni kati ya 14 wanaohojiwa kuhusiana na kisa hicho kilichosababisha kuteketea kwa bweni hilo lenye uwezo wa kuwahifadhi wanafunzi 160, na Shule yao kwa sasa imefungwa.
Social Plugin