Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Shilela, Bi. Rahabu Nkwabi akielezea namna tabia ya wanaume kulala na wake zao huku wamevaa suruali inavyochangia ukatili wa kingono.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wanawake katika kata ya Shilela halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga wamewaomba wanaume kubadilika na kuacha kuwafanyia ukatili wa kingono wake zao kwa kutowapatia haki yao ya ndoa kwa kulala wakiwa wamevaa suruali.
Hayo yamesemwa leo Jumatano Septemba 30,2021 na Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Shilela kinachosimamiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Rahabu Nkwabi wakati wa mkutano wa hadhara katika kata hiyo kujadili tathmini ya matukio ya ukatili wa kijinsia.
Rahabu alisema matukio ya ukatili wa kijinsia katika familia nyingi yamekuwa yakisababishwa na tabia za wanandoa kuanza kusaliti wenza wao matokeo yake wanashindwa kuwapatia haki ya ndoa wake zao hali inayosababisha nao kuanza kuchepuka ili kukidhi haja zao za kimwili.
“Wanawake vunjeni ukimya, fungukeni kuhusu akina baba wanaolala na suruali kwani wanawafanyia ukatili wa kingono kwa kuwanyima haki yenu ya ndoa", amesema Rahabu.
“Mwanaume kwanini ulale na mke wako huku umevaa suruali? ulioa kwa ajili ya nini,huoni kuwa unamnyima haki yake mkeo na kumfanya awaze kuwa unamsaliti kwa kufanya ngono na wanawake wengine nje ya ndoa. Kwanini ulale na suruali wakati mwenzako anataka, umeshiba huko nje ndiyo maana ndani hutaki?”,amehoji Rahabu.
Katika hatua nyingine Rahabu aliwataka akina mama kuwapatia haki ya ndoa waume zao na kuepuka visingizio na sababu za mara kwa mara kuwa hawawezi kushiriki tendo la ndoa kwani kitendo cha kunyimana tendo la ndoa kinasababisha migogoro hali inayopelekea kupigana ndoa kuvunjika na kusababisha watoto kuteseka, kutelekezwa na kuacha shule,kuolewa wangali wadogo au kuzurura tu mtaani.
“Wanawake wapeni tendo la ndoa waume zenu, acheni visingizio. Mkiwanyima ndiyo maana wengine wanaamua kuanza kuchepuka matokeo yake wanalala na suruali. Wanaume nanyi na msipowapa haki yao wake zenu inafikia wanawake wanachoka kuvumilia wanatafuta wanaume wa pembeni kisha mnaanza kuvurugana humo ndani ya nyumba”,ameongeza Rahabu.
Aidha amewashauri akina mama kutoa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia badala ya kukaa tu kimya huku akiishauri jamii kuacha tabia ya kuozesha watoto wadogo.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Shilela Shiminzi Ngeleja amesema suala la wanandoa kunyimana tendo la ndoa limekuwa chanzo cha matukio ya ukatili ndani ya familia hali inayojenga chuki na kusababisha migogoro ya hapa na pale hivyo ni vyema pande zote (mke na mme) kukaa chini na kutatua changamoto zao.
"Hili suala la kunyimana tendo la ndoa lipo pande zote mbili, tunapokea kesi kwa baadhi ya wanaume wanalala na wake zao huku wakiwa wamevaa suruali, wanawake nao wanakwepa tendo kwa visingizio vingi na wapo wanalala huku wamevaa suruali/ Skin tight (Jeans za kubana) kiasi kwamba huwezi kumvua, huu ni ukatili wa kingono na wanapata sana athari za kisaikolojia matokeo yake ugomvi ndani hauishi", amesema Ngeleja.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Shilela Bi. Mwanaidi Mustapha Mzee amesema amekuwa akipata kesi mbalimbali kwa baadhi ya wanandoa kunyimana tendo la ndoa ambapo kesi hizo huwa wanazipeleka kwenye Baraza la usuluhishi la kata.
“Nimekuwa nikipokea kesi za wanandoa kunyimana tendo la ndoa. Hivi karibuni nimepata kesi kuhusu mwanaume kulala na mke wake huku akiwa amevaa suruali kwa muda wa miezi miwili mfululizo,mwanamke akavumilia. Lakini cha kushangaza mwanaume huyo akaanza kumpiga mkewe ili aondoke aoe mwanamke mwingine”,amesema Mwanaidi.
Amesema matukio ya wanaume kuwapiga na kuwafukuza wake zao yamekuwa yakitokea hasa katika kipindi cha mavuno ambapo baadhi ya wanaume wanaanza kufanya vituko ili kutumia peke yao mali walizochuma na wake zao.
Hata hivyo amesema wanaendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu Ukatili wa kijinsia ili watu wabadilike, waishi kwa amani na upendo ili kuchochea maendeleo katika jamii sambamba na namna ya kupata haki zao pindi zinapopotea au zinapotaka kupotea.
Kwa upande wake, Mkazi wa Shilela Simon Masolwa amesema tabia ya watoto kusindikiza Harusi inasababisha ukatili wa kijinsia kwani watoto wanaanza kujifunza mambo ya wakubwa na kujikuta wanaolewa au kupata mimba wangali wadogo.
Katibu Msaidizi wa Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Shilela, Joseph Samwel Mbunge amesema miongoni mwa mafanikio yaliyofikiwa na kituo hicho ni pamoja na kupunguza ndoa za utotoni na kurudisha shuleni watoto walioacha masomo yao.
Msaidizi wa Kisheria Esther Mwampashi kutoka kata ya Bulige amewashauri wanajamii kuvunja ukimya juu ya matukio ya ukatili wa kijinsia na kuibua matukio mbalimbali yaliyofichwa ili yaweze kutatuliwa na wasaidizi wa kisheria na waragbishi na wana vituo vya taarifa na maarifa.
Naye Afisa Tathmini na Ufuatiliaji wa Shirika la linalotoa msaada wa kisheria mkoani Shinyanga Paralegal Aid Centre (PACESH), Henerico Masasi amewataka wanajamii kuwatumia wana vituo vya taarifa na maarifa na wasaidizi wa kisheria kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo mimba na ndoa za utotoni na migogoro ya ndoa na ardhi.
Mkutano huo wa hadhara uliolenga kutoa Matokeo ya Utekelezaji wa Shughuli za Mradi wa Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wanawake kiuchumi unaotekelezwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kupitia shirika la Watu na Makazi Duniani (UNFPA tangu mwezi Julai 2020.
Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Shilela kinachosimamiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Rahabu Nkwabi akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kata hiyo kujadili tathmini ya matukio ya ukatili wa kijinsia Septemba 30,2021.Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Shilela kinachosimamiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Rahabu Nkwabi akiwasihi wanawake na wanaume kuvunja ukimya kwa kutoa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia ikiwemo ukatili wa kingono kwa kunyimana tendo la ndoa.
Wananchi wa kata ya Shilela halmashauri ya wilaya ya Msalala wakiwa kwenye mkutano wa hadhara katika katika kijiji cha Shilela kujadili tathmini ya matukio ya ukatili wa kijinsia
Wananchi wa kata ya Shilela halmashauri ya wilaya ya Msalala wakiwa kwenye mkutano wa hadhara katika katika kijiji cha Shilela kujadili tathmini ya matukio ya ukatili wa kijinsia
Afisa Mtendaji wa Kata ya Shilela Bi. Mwanaidi Mustapha Mzee akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika katika kijiji cha Shilela kujadili tathmini ya matukio ya ukatili wa kijinsia katika kata ya Shilela halmashauri ya wilaya ya Msalala.
Mkazi wa Shilela Simon Masolwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika katika kijiji cha Shilela kujadili tathmini ya matukio ya ukatili wa kijinsia katika kata ya Shilela halmashauri ya wilaya ya Msalala.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Shilela Shiminzi Ngeleja akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika katika kijiji cha Shilela kujadili tathmini ya matukio ya ukatili wa kijinsia katika kata ya Shilela halmashauri ya wilaya ya Msalala.
Msaidizi wa Kisheria Esther Mwampashi kutoka kata ya Bulige akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika katika kijiji cha Shilela kujadili tathmini ya matukio ya ukatili wa kijinsia katika kata ya Shilela halmashauri ya wilaya ya Msalala.
Afisa Tathmini na Ufuatiliaji wa Shirika la linalotoa msaada wa kisheria mkoani Shinyanga Paralegal Aid Centre (PACESH), Henerico Masasi akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika katika kijiji cha Shilela kujadili tathmini ya matukio ya ukatili wa kijinsia katika kata ya Shilela halmashauri ya wilaya ya Msalala.
Wananchi wa kata ya Shilela halmashauri ya wilaya ya Msalala wakiwa kwenye mkutano wa hadhara katika katika kijiji cha Shilela kujadili tathmini ya matukio ya ukatili wa kijinsia
Igizo kuhusu Ukatili wa Kisaikolojia likiendelea kwenye mkutano wa hadhara ambapo jamaa amenaswa mubashara akimchungulia mwanamke anayeoga bafuni hali inayomfanya mwanamke huyo aathirike kisaikolojia kuchunguliwa
Katibu Msaidizi wa Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Shilela, Joseph Samwel Mbunge
Wasaidizi wa Kisheria halmashauri ya wilaya ya Msalala wakiwa kwenye mkutano wa hadhara katika katika kijiji cha Shilela kujadili tathmini ya matukio ya ukatili wa kijinsia
Social Plugin