WATU wanne wamefariki dunia na wengine saba wamejeruhiwa kwenye ajali ya barabarani iliyohusisha lori na basi la Isamilo, lililokuwa linasafiri kutoka mkoani Mwanza kuelekea mkoani Mbeya.
Mkuu wa wilaya ya Iringa, Mohamed Moyo amesema ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Izazi kilichopo tarafa ya Isimani wilayani Iringa.
Amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Iringa, huku majeruhi saba wa ajali hiyo wakiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo.
Chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi, ambapo dereva wa lori alijaribu kulipita gari la mbele yake, na hivyo kuligonga basi la abiria uso kwa uso.
Jeshi la Polisi mkoani Iringa, linamsaka dereva wa lori aliyesababisha ajali hiyo, ambaye alitokomea kusikojulikana mara baada ya kusababisha ajali.
Social Plugin