Na. WAMJW-Nairobi
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima jana ameshiriki mkutano wa uzinduzi wa kituo cha kanda ya mashariki mwa Afrika kinachoshughulikia udhibiti wa magonjwa (EA Regional Collaboration Centre) kinachosimamiwa na kituo cha udhibiti wa magonjwa Afrika (Afrika CDC).
Kituo hiki kinaratibu na kuimarisha udhibiti wa magonjwa ya milipuko na yale yenye umuhimu katika jamii na kinatarajiwa kujengea uwezo wataalam wa afya ya jamii,kuimarisha taasisi za kitaifa za afya ya jamii, kuanzisha mtandao wa kikanda wa ufuatiliaji wa magonjwa na huduma za kimaabara pamoja na kuimarisha uzalishaji wa ndani wa bidhaa za afya.Kituo cha EARCC kinajumuisha nchi 14 ambazo ni Tanzania, kenya , Uganda ,Rwanda, Burudi, DRC, South Sudan, Djiobut, Sudan, Somalia, Comoro, Sychalles, Madagascar ,Eriteria na Ethiopia.
Uanzishwaji wa kituo hiki unafuatia maazimio ya wakuu wa nchi za Afrika walipokutana kwenye kikao cha mwaka 2015.