ALIYEKUWA Naibu Waziri wa Uwekezaji na Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro William Tate Ole Nasha amezikwa jana Oktoba 02 2021 katika kijiji cha Osnoni Wilaya ya Ngorongoro
Miongoni mwa viongozi waliohudhuria mazishi hayo ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,Spika wa Bunge Job Ndugai,Katibu wa Siasa na Itikadi wa Chama cha Mapinduzi Shaka Hamdu Shaka ,Mawaziri na Manaibu Mawaziri,pamoja na Wabunge.
Majaliwa ambaye ameshiriki katika mazishi hayo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kifo cha Ole Nasha ni pigo kubwa kwa Serikali, Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bunge pamoja na kwa wanafamilia na wananchi wa Ngorongoro
Social Plugin