Na Emmanuel Mbatilo
Klabu ya Yanga imeendelea kutembeza kichapo katika Ligi Kuu ya NBC mara baada ya leo kufanikiwa kuonddoka na pointi tatu kwa kuwachapa KMC Fc 2-0 katika dimba la Majimaji Songea Mkoani Ruvuma.
Ni Feisal Salum (Fei Toto)ambaye alionekana moto katika mchezo huo ambapo alicheza soka la aina yake kwa kufanikisha kutengeneza baoo lililofungwa na Fiston Mayele dakika ya 4 ya mchezo.
Dakika ya 11 tena Feisal alifanikiwa kupata bao kwa kuachia shuti kali lililomshinda Faroukk Shikalo na kuingia moja kwa moja wavuni.
Kipindi cha pili mchezo ulibadilika kwa kiasi kikubwa licha ya Yanga kucheza soka murua kipindi cha kwanza lakini kipindi cha pili kulibadilika ikawa KMC Fc kulikamata dimba la kati na muda mwingi wakawa wanatawala mchezo licha ya kutopata bao katika mchezo huo.
Social Plugin