Na Dotto Kwilasa, Malunde 1 blog Dodoma
Naibu Spika Dk.Tulia Ackson amelitaka Shirika la ndege nchini (ATCL) kuhakikisha linajiendesha kwa tija na faida ili kuondoa dhana iliyojengeka kwa baadhi ya watu kuona linajiendesha kwa hasara.
Naibu Spika Dk.Tulia Ackson amesema hayo leo Jijini Dodoma mara baada ya kukutana na kamati mbalimbali za Bunge na shirika hilo ambapo amesema changamoto zinazosemwa kama zikifanyiwa kazi ni wazi zitaleta mabadiliko chanya kwa wananchi.
Dk. Tulia alisema ATCL Ina jukumu la kuhakikisha linakidhi mahitaji ya watanzania kwa kujiendesha kisasa ikiwa ni pamoja na kuondoka kero zote zinazolikabili shirika hilo.
"Mashirika yetu haya kama yatasimamiwa vizuri yatakuwa na tija na yataleta mafanikio chanya kwa Taifa letu,
Pia sisi kama bunge tutakuwa karibu na Shirika letu hili ili kuweza kuona kwa ukaribu changamoto zinazoikabili Shirika letu,"amesema Tulia.
Aidha amesema wabunge kama wawakilishi wa wananchi walipata uelewa juu ya shirika la ndege la Taifa litawapa uelewa kwani wakielewa wao wanachi pia wataelewa kwani watakuwa mabalozi Wazuri kwa kulisemea Shirika.
"Tukipata uelewa sisi ni rahisi sana kuwa mabalozi hasa kwa kuwaelimisha wananchi wetu na wao waweze kuwa na uelewa juu ya shirika letu hili la ndege,"ameeleza Naibu Spika.
Social Plugin