Wakati unazuru baa, ikiwa wahudumu wanaonyesha urafiki na wanasaidia, inaongeza zaidi starehe zako. Lakini wakati unakutana mhudumu wa baa asiye mchangamfu huwa inapunguza kiwango cha starehe zako.
Kwa watu walio na maeneo fulani ambapo wao hunywa mara kwa mara, mtu anayetoa huduma anaweza kuwa rafiki na hata mtu wa kuamini.
Lakini hivi karibu wahudumu hao wa baa hawatakuwa wanadamu. Cecilia, roboti mhudumu wa baa anayechanganya na kuwapa wateja vinywaji, na kutumia akili bandia kuzungumza na wateja ni sawa na vile Alexa kwenye vipasa sauri vya Amazon au Siri kwa simu ya Iphone anaweza kukujibu.
Kifaa hicho huonekana kama mashine refu ya matunda, na picha ya mwanamke mhudumu Cecilia wa baa huonekana kwenye skrini kubwa. Unaweza kumuambia ni kinywaji gani unakitaka au kuitisha kinywaji kwa kutumia skrini iliyo chini yake na ulipe kinywaji chako kwa kutumia kadi ya banki au simu.
Je wahudumu wa baa wanapaswa kuwa na hofu ya kazi zao?
Kisha kinywaji chako kinachanganywa ndani ya mashine na kisha kunatirika kwenda glasi.
"Cecilia hufanya kazi kwa kutambua sauti na teknoljia ya AI," anasema Elad Kobi, mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Israel iliyobuni teknolojia hiyo - Cecilia.AI. Anaweza kuzungumza na wateja, na awakati wanachagua kinywaji fulani anaweza kukitengenwza moja kwa moja."
Kampuni inasema kuwa kila mashine inaweza kujazwa na lita 70 za mvinyo tofauti na kwanza inaweza kuhudumia hadi watu 120 kwa saa. Kama wateja hawatakaa kwa mazungumzo zaidi.
Kampuni ilitoa roboti hiyo mwanzo mwa mwezi Februari tarehe 24 mwaka huu - siku ya wahudmua wa baa duniani. Tangu wakati huo imetumiwa kwenye warsha za mashirika ambazo zimaendaliwa na kampuni za Microsoft, KPMG na Cisco. Wateja wanaweza kununuaa Cecilia kwa dola 45,000 na kukodi kwa kwa dola 2,000 kwa mwezi.
Bw. Kobi anaamini kuwa baa ambazo hazitaki kubadilisha mfumo kitamaduni zinaweza kugeukia teknolojia hiyo kama njia ya kuwavutia wateja.
"Kampuni hugundua kuwa zinahitajika kufanya mambo kwa anjia tofauti na wengine kuwavutia wateja," anasema. Teknoljia na uvumbizi vinaweza kuyafanya hayo. Cecilia.AI pia inalenga hoteli, viwanja vya ndege, viwanja vya michezo, kasino na meli za abiria.
Waunga mkono roboti za baa pia wanasema kuwa wanaweza kusaidia baa kuwa na huduma bora.
Alan Adojaan anasema kuwa, kuna wakati katika vilabu hasa vya usiku wateja hawataki kuzungumza na mhudumu wa baa
"Suala kuu ni wakati kuna baa ambayo labda inakumbwa na matatizo ya kila mara kuhusu wafanyakazi," anasema Alan Adojaan. Yeye ni mkurugenzi mkuu wa Yanu, kampuni kutoka Estonia ambayo hivi majuzi ilizindua roboti ya kuhudumu kwenye baa.
Kila mara kuna uhaba wa wafanyakazi. Lazima uwape mafunzo lakini wao huondoka.
Anasema roboti wafanyakazi wa baa watatatua tatizo hili na mambo mengine kama kuweka kinywaji kingi kupita inavyostahili au kutoa vinywaji wa bure kwa marafiki .
"Tunalenga maeneo yenye wateja wengine, kwa mfano warsha za michezo, sherehe na vilabu vya usiku," anasema. Mashine hizi zinafanya kazi kwa haraka sawa na wahumu watatu unusu wa baa na kutengeneza vinywaji 100 kwa saa."
Kando na hilo roboti za kuhudumu kwenye baa zinaweza kufanya kazi saa 24 katika mazingia ambayo yatakuwa magumu kwa mwanadamu kufanya hivyo.
Makampuni yanasema baadhi ya wahudumu roboti wanaweza kufanya kazi haraka na kuwa inayoweza kufanywa na wafanyakazi watatu na nusu wa baa ambao ni binadamu na wanaweza kuhudumia vinywaji 100 kwa saa.
Kama ilivyo katika sekta zingine, kuongejea wa roboti kuhudumu kwenye baa inaleta wasi wasi wa kupotea ajira.
Emanuele Rossetti, mkuu wa kampuni ya kutengeneza roboti za kuhudumu kwenye baa Makr Shakar anasema iwapo baadhi ya wafanyakazi wa baa watapoteza ajira, wanaweza kupata kazi zingine katika sekta kubwa ya ukarimu.
Kumsaidia mfanyakazi wa baa ambaye aliathiriwa, ilianzisha mpango nchini Marekani mwaka 2019 ambapo kwa kila roboti inauzwa watampa mfanyakazi dola 1000 kumsaidia kupata mafunzo mapya.
"Roboti haziwezi kuchukua nafasi ya wanadamu," anasema Jan Hiersemenzel, mkuu wa masoko katika kampuni ya roboti ya uswizi F&P Robotics inayounda roboti kwa jina Barney Bar.
F&P Robotics inasema roboti kama hizo hazitachukua nafasi za wafanyakazi wengi wa baa.
Baa za Uingereza JD Wetherspoon hazina mpango wa kununua roboti hizo kufanya kazi kwenye baa zake. Kulingana msemaji wake, kampuni hiyo inasema haiwezi kufanya hivyo.
Lakini Bw Adojaan kutoka Yanu anasema ana uhakika kwa kuwepo mauzo kwa baa za kawaida na vilabu vya usiku.
Kwa wateja wanaopenda kuzungumza na wahudumu wa baa, Bw Adojaan anasema roboti zinaboreka zaidi na kuwa na tabia sawa na za mwanadamu.
"Tunajaribu kuunda kitu fulani.. kinachoweza kushiriki mazungumzo, au kufanya mzaha na kuuliza ikiwa uliikipenda kinywaji chako, au kupendekeza kinywaji kingine," anasema.
Chanzo - BBC Swahili
Social Plugin