Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KIVULINI, POLISI NA MANISPAA YA ILEMELA WAZINDUA KAMPENI YA BODABODA KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA...WAENDESHA BODA WAONYWA MAPENZI NA WANAFUNZI

Na Mwandishi wa Malunde 1 blog Mwanza
Shirika la kutetea haki za wanawake na watoto la KIVULINI kwa kushirikiana na halmashauri ya manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza pamoja na Jeshi la Polisi wilayani Ilemela imezindua Kampeni ya bodaboda inayolenga kutokomeza mimba za utotoni na ndoa za utotoni na ukatili wa kijinsia katika wilaya ya Ilemela.

Akizungumza leo Ijumaa Novemba 5,2021 wakati wa Uzinduzi wa Kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Shirika la Kivulini Yassin Ally amesema kampeni hiyo inalenga kuwashirikisha bodaboda kama Wakala wa Mabadiliko katika kutokomeza tatizo la mimba pamoja na ndoa za utotoni kufuatia baadhi yao kudaiwa kuwa chanzo cha tatizo hilo.

Ameongeza kuwa kampeni hiyo inalenga kuwafanya bodaboda kujitambua katika malengo yao binafsi ya maisha pamoja na kuchangia katika maendeleo ya taifa ikiwa ni pamoja na kuwa mabalozi wazuri wa kutokomeza mimba za utotoni, ndoa za utotoni na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.

Ally ameendelea kusisitiza kuhusu Kauli mbiu ya 'Chapa Kazi Siyo Mkeo na Kama Unapenda Sketi za Shule, Mshonee Mkeo', Funguka! Muwezeshe asome usimpe mimba'.

Akizindua kampeni hiyo,Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Renatus Mulunga amewataka waendesha bodaboda kuzingatia kanuni,taratibu na sheria katika utekelezaji wa majukumu yao pamoja kuwa waadilifu katika maisha yao ya kila siku huku wakiwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya matukio ya ukatili wa kijinsia.

Mulunga amewaasa waendesha bodaboda kujiunga katika vikundi ili waweze kunufaika na mikopo isiyokuwa na riba inayotolewa na manispaa hiyo pamoja na kujiwekea akiba ili kupata mitaji ya kuwekeza kwenye shughuli mbalimbali za kujiongezea kipato.

Kwa upande wake, Mkuu wa Polisi wa wilaya Ilemela Mrakibu mwandamizi wa polisi Elisante Ulomi amewatahadharisha waendesha bodaboda wanaojihusisha na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi.

Ulomi amewaasa waendesha bodaboda kuwafichua wanaojihusisha na mapenzi na wanafunzi ili hatua stahiki za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Nao baadhi ya waendesha bodaboda wamekiri baadhi yao kujihusisha na vitendo vya uhalifu ikiwemo kukwapua mikob ya abiria hususani wanawake pamoja na kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi.

Aidha wameiomba serikali kukomesha uwepo wa wimbi la waendesha bodaboda wasiokuwa na vituo maalum ambao wamedai kuwa vinara wa uhalifu pamoja na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi.

Pia wameomba Shirika la Kivulini liwapatie elimu ya kujitambua mara kwa mara ili waweze kuwa mabalozi wema zaidi wa kutokomeza mimba na ndoa za utotoni pamoja na ukatili wa kijinsia.

Waendesha bodaboda 135 kutoka kata mbalimbali za manispaa ya Ilemela zikiwemo Buswelu, Nyamhongolo na Kahama wamepatiwa viakisi mwanga (Reflectors) wakati wa uzinduzi wa kampeni ya bodaboda inayolenga kutokomeza mimba za utotoni pamoja na ukatili wa kijinsia katika wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza ambapo mratibu wa sekta isiyo rasmi katika manispaa hiyo Raphael Mfuru amewahimiza kuzitumia kwa malengo yaliyokusudia ili kuleta matokeo chanya.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Renatus Mulunga akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya bodaboda inayolenga kutokomeza mimba za utotoni pamoja na ukatili wa kijinsia katika wilaya ya Ilemela. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Kivulini, Yassin Ally
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Renatus Mulunga akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya bodaboda inayolenga kutokomeza mimba za utotoni pamoja na ukatili wa kijinsia katika wilaya ya Ilemela.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Renatus Mulunga akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya bodaboda inayolenga kutokomeza mimba za utotoni pamoja na ukatili wa kijinsia katika wilaya ya Ilemela. Katikati ni Mkuu wa polisi wilaya Ilemela Mrakibu Mwandamizi wa polisi Elisante Ulomi , kulia ni  Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Kivulini, Yassin Ally
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Renatus Mulunga akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya bodaboda inayolenga kutokomeza mimba za utotoni pamoja na ukatili wa kijinsia katika wilaya ya Ilemela. Katikati ni Mkurugenzi wa Shirika la Kivulini, Yassin Ally , kulia ni Mratibu wa Sekta isiyo rasmi manispaa ya Ilemela Raphael Mfuru 
Mkurugenzi wa Shirika la Kivulini, Yassin Ally akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya bodaboda inayolenga kutokomeza mimba za utotoni pamoja na ukatili wa kijinsia katika wilaya ya Ilemela.
Mkurugenzi wa Shirika la Kivulini, Yassin Ally akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya bodaboda inayolenga kutokomeza mimba za utotoni pamoja na ukatili wa kijinsia katika wilaya ya Ilemela.
Mkurugenzi wa Shirika la Kivulini, Yassin Ally akitoa mafunzo kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya bodaboda inayolenga kutokomeza mimba za utotoni pamoja na ukatili wa kijinsia katika wilaya ya Ilemela.
Mratibu wa sekta isiyo rasmi halmashauri ya manispaa ya Ilemela Raphael Mfuru akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya bodaboda inayolenga kutokomeza mimba za utotoni pamoja na ukatili wa kijinsia katika wilaya ya Ilemela.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani wilayaIlemela Celestine Lusendelo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya bodaboda inayolenga kutokomeza mimba za utotoni pamoja na ukatili wa kijinsia katika wilaya ya Ilemela.
Dereva wa bodaboda akiwa na bango la kupinga ukatili wa kijinsia 'Chapa Kazi Siyo Mkeo'

Dereva wa bodaboda akiwa na bango la kupinga ukatili wa kijinsia


Dereva wa bodaboda akiwa na bango la kupinga ukatili wa kijinsia 'Chapa Kazi Siyo Mkeo'
Dereva wa bodaboda akiwa na bango la kupinga ukatili wa kijinsia 'Chapa Kazi Siyo Mkeo'

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com