COSTECH KUENDELEA KUUNGA MKONO UBUNIFU KWA VIJANA KUINUA UCHUMI WA VIWANDA


Na  Dotto Kwilasa, Malunde 1 blog Dodoma.
ILI kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuchochea  uchumi wa viwanda,Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imesema inaendeleza jitihada za kufanya uatamizi wa mawazo ya vijana na watu Wenye Teknolojia ya ubunifu ili kuwawezesha kuziishi ndoto zao.

Ofisa Uhusiano wa COSTECH Mary Kigosi amesema hayo hivi karibuni jijini Dodoma wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya ubunifu yaliyoandaliwa na  Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kushirikiana SIDA ambayo yamefanyika kwa siku mbili.

Kigosi amesema watu wengi wamefanikiwa baada ya ufadhiri wa taasisi hiyo inayowabeba kwenye utafiti, ubunifu na huduma lakini walengwa zaidi huwa ni vijana.

"Kuna vijana wengi wana ndoto kubwa lakini hawana uwezo wa kuzifikia kutokana na kushindwa kugharamia, tunatumia nafasi hiyo kuwasaidia kutimiza ndoto zao kwa uchumi wa viwanda,"alisema.

Kutokana na hayo Mkurugenzi mwenza wa JV Biotech Enterprise Co Ltd  Jacob Tito ambaye pia ni mnufaika amewashauri vijana wenye ujuzi Kuona haja ya kuwasiliana na Costech  ili kuwawezesha kwamba kwa kufanya hivyo wataisaidia jamii kuondokana na tatizo la ajira.

Ametaja baadhi ya hatua wanazopitia hadi kuyafikia mafanikio kwamba zina kikwazo vingi akaomba zitazamwe .

"Mimi ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam namiliki kiwanda Cha kusindika mazao ya muhogo baada ya kuwezeshwa mtaji na Tume ya Taifa ya sayansi na teknojia ( COSTECH),naamini kuna vijana wenzangu wengi wabunifu lakini wanashindwa namna ya kutimiza ndoto zao;

Niwashauri waje washirikiane na tume hii ya sayansi na wataona matunda yake,uchumi wa Viwanda unatutegemea Sana vijana hakuna haja ya kuchelewa,"amesisitiza.

Mbali na hayo Tito ametaja moja ya eneo ambalo amesema limekuwa na ucheleweshaji mkubwa na hata kuondoa ndoto za vijana ni kwenye uthibitisho wa ubora ambao vibali vyake hutolewa na Shirika la viwango Tanzania (TBS).

"Bila kuwezeshwa na Costech yani tungekwama kufikia ndoto zetu, sisi ni vijana wawili ambao tulimaliza masomo yetu Chuo Kikuu UDSM, lakini tukaona tujiajiri sisi ndiyo tukakutana na mlolongo wa mambo hadi inakatisha tamaa," anasema Jacob.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, hivi sasa wameajiri vijana wenzao 5 na vibarua wa Kila siku wako 25 baada ya wazo lao kukubaliwa na kupokelewa na Costech kisha wakasaidiwa Sh40 Milioni.

Naye Notkery Mwalongo ambaye alisaidiwa kufanya utafiti wa namna ya kuua Gugu Kongwa katika ranchi ya migugo, alisema uwezeshwaji kwa ajili ya vijana umekuwa mkombozi na kuondoa fikra za kuajiriwa.

Mwalongo amesema kazi aliyofanya kwa msaada tume hiyo ina manufaa makubwa kwa wafugaji ambao wamekuwa wakipoteza sehemu kubwa ya malisho yao baada ya Gugu hilo kuota.

Aidha ameimeomba Serikali kutazama gharama za baadhi ya taasisi zake ambazo zinatoa vibali kwa wajasiliamali kwani zinakuwa kikwazo kwa mafanikio yao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post